Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa mitandao wa TTCL 4G LTE katika Mkoa wa Iringa eneo la ofisi za kampuni hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizindua huduma ya mtandao wa simu wa TTCL kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa bi Amina Masenza
Na fredy Mgunda, Iringa.
Watanzania wametakiwa kuanza
kuutumia mtandao wa simu wa TTCL kwa kuwa umeboreshwa kwa kiwango kikubwa na
huduma zao zinazingatia wateja wake ili kuendelea kiinufaisha serikali kwa kuwa
mtandao huo unamilikiwa na serikali.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa TTCL 4G mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema kuwa
wananchi wanapaswa kuunga mkono mtandao huu wa kizalendo ambao unahuduma nyingi
nzuri.
“Ukiangalia utagundua kuwa
mtandao wa TTCL inahuduma ya pesa ambazo zina makato madogo sana kulinganisha
mitandao mingine hivyo nawasiii wananchi wa mkoa wa iringa kuanza kutumia
huduma za mtandao huu wa kizalendo” alisema Abdallah
Abdallah aliwataka wananchi
kuanza kuvithamini vitu vya wazawa kwanza ili kuleta maendeleo ya maendeleo
kwenye kampuni na taasisi za kizalendo
ndio maana mkuu wa mkoa wa Iringa na wakuu wa wilaya wote wa mkoa huu
wameamua kujiunga na mtandao huu wa TTCL.
“Mimi,mkuu wa mkoa ,mkuu wa
wilaya Richard Kasesela na viongozi
wengine wamejiunga na mtandao huu wa TTCL 4G ambao unakasi kubwa kwenye upande
wa internet na huduma nyingine ziboreshwa na zimekuwa bora sana” alisema
Abdallah
Aidha Abdallah alisema kuwa
kampuni hii ya kizalendo imekuwa ikihudumia jamii kwa njia tofautitofauti za
kimaendeleo hasa kwa kuunga mkono kwenye michezo mbalimbali hapa nchini.
“Kama unakumbuka hivi
karibuni kulikuwa na mshindano ya Ritta kabati challenge cup ambapo kampuni hii
ya kizalendo ilichangia zaidi ya milioni mbili kufanikisha kuendesha mashindano
hayo hivyo utagundua kuwa TTCL imekuwa ikirudisha faida kwa wananchi”alisema
Abdallah
Abdallah alisema kuwa TTCL
wana bando kuwa kwa gharama nafuu hivyo naomba wananchi wanaopenda kutumia
mitandao ya kijamii wanapaswa kujiunda na mtandao huu kwa kuwa unagharama nafuu
na internet yake inakasi nzuri kulingana na mitandao mingine.
Kwa upande wake mkurugenzi
mkuu wa Kampuni ya TTCL nchini Waziri Kandamba alisema kuwa TTCL imekuja
kuboresha maisha ya watanzania wanaopenda kutmia mitandao ya simu kwa kuwa
wamejipanga kufanya kazi kishindani tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
“Leo tumefanya uzinduzi wa
mtandao wenye kasi kubwa 4G LTE ambao utakuwa unakata kiu kwa wanaopenda
kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwa tumeboresha huduma zetu zote katika
mtandao huu” alisema kandamba
Kandamba aliwataka
watanzania kuvitumia na kuvithamini vitu vya kwao kama makampuni ya wazao ndio maana TTCL ilirudi kuwatumikia
watanzania kwa kuboresha huduma zetu zote.
“Wewe jaribu kutumia mtandao
wetu wa TTCL utapata jibu zuri kwa kiasi gani tumeboresha huduma hii ambayo
watanzania wengi waliikosa kwa muda mrefu hivyo nawaomba watanzania kujiunga na
mtandao wetu wa TTCL wenye huduma bora” alisema Kandamba
No comments:
Post a Comment