ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, August 29, 2017
LISSU AWAONGOZA MAWAKILI KUGOMA KUINGIA MAHAKAMANI
RAIS wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu amewaongoza mawakili nchini kugoma kuingia mahakamani kwa muda siku mbili leo Agosti 29 na 30, 2017 wakilaani tukio la kushambuliwa kwa ofisi za IMMMA Advocates iliyolipuliwa kwa bomu usiku wa kumakia Jumamosi iliyopita.
Akizungumza na wanahabari kuhusu uamzi wa Baraza la TLS, Lissu amesema ni haki ya kisheria ya mtu yeyote kutoa maoni yake, kupinga maamuzi ya TLS, sio dhambi na hatochukuliwa hatua.
“Mengi wamefanyiwa mawakili lakini hili la juzi tumesema hatukubali kukaa kimya wakati mawakili wetu wanashambuliwa. Kwa busara za TLS tuliona tufanye maamuzi ya kusimamisha kazi kwa siku mbili ili kupeleka ujumbe kuwa jambo hilo si jema,” alisema Lissu.
Kuhusu endapo mawakili wote wamegoma Lissu alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa, hadi jioni ambapo ripoti kamili itakuwa imepatikana kwa kuwa kuna mawakili wengine walikuwa na kesi asubuhi, wegine mchana, hivyo haikuwa rahisi kufahamu ni mawakili wangapi wamegoma. GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
hawa mawakili wao na rais wao wanamgomea nani sasa wateja wao? kwani wao ndio wamelipua hilo bomu. kujaaliwa akili ni neema lakini kukosa kuitimia kwa busara ni balaa
Post a Comment