ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 28, 2017

SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU WILSON CHARLES AMOUR

Sarah, Tivan Amour,Sabrina Ally, Khadija Abdullah wa New York City, Biubwa Marumbo wa Takoma na Alban Abdul-aziz wa Texas tunawashukuru wote walioweza kuungana nasi na hata wale walioshindwa kwa sababu mbalimbali katika ibada maalumu ya kumuombea ndugu yetu Wilson Charles Amour iliyofanyika Siku ya Jumamosi Takoma Park. 

Kwa namna ya pekee tunamshukuru kiongozi wa mtandao unaoheshimika "Vijimambo Blog" Luke Joe na timu yake nzima kwa kuchukua muda wake mwingi kusambaza taarifa mbalimbali za msiba huu hadi pale tulipousafirisha nyumbani Zanzibar kwa mazishi. Ahsante sana Luke. 

Mwisho tunawashukuru wale wote waliotuma salamu mbalimbali za kutufariji katika kipindi chote cha majonzi Asanteni sana na tumefarijika sana. Tunaomba kwa imani zetu kila mmoja amuombe Mwenyezi Mungu aipokee roho ya mjomba wetu. Raha ya milele umjaalie ee Mungu na Mwanga wa daima umwangaze. Astarehe kwa amani Marehemu Wilson Charles Amour. Ameen



1 comment:

Anonymous said...

poleni sana sana kabisa wafiwa wote,ndugu na jamaa na marafiki.Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi uncle Charles amour.Amen .Mwenyezi mungu akupeni moyo wa subrah wafiwa wote.

To God we came to him we shall return.