ZAIDI ya wakazi 3000 wanaoishi
katika eneo la Jaribu tena na Mwisho wa Shamba kata ya Maweni Jijini
Tanga wanatarajiwa kuepukana na adha ya uhaba wa maji safi na salama uliyodumu kwa muda mrefu baada ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa
mazingira Jijini Tanga kuwa pelekea mradi wa maji.
Akizungumza na waandishi wa habari
Mkurungenzi Mtendaji wa Tanga UWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema
kuwa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka
huu.
Alisema kuwa gharama za mradi huo
hadi kukamilika kwake ni kiasi cha sh Mil98,lakini kutoka na gharama
kuwa kubwa waliwashauri wananchi ili kuona namna watakavyoweza kufanya
kazi za kujitolea ili kukamilika kwa wakati.
Alisema kuwa ndipo wananchi
walipoamua kushiriki katika kazi za kuchimba mitaro ambayo itaweza
kutumika kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya mabomba kutoka Pongwe
hadi katika maeneo hayo yenye uhitaji.
“tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano waliounyesha wa kushiriki kwenye uchimbaji huo kwani wameweza kuokoa kiasi cha sh Mil 10 ambazoingebidi tuwalipe vibarua kwa ajili ya uchimbaji wa mitaro hiyo”alisema Mgeyekwa.
Alisema kuwa mradi huo
umegawanyika katika awamu ambapo katika awamu ya kwanza unatarajiwa
kusambaza maji katika umbali wa Km 5.5 kutoka eneo la Pongwe hadi katika
mitaa ya Jaributena na Mwisho wa shamba.
Nae Mbunge wa Jimbo la Tanga Mussa Mbaruku alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kwa haraka kutaweza kusaidia wananchi hao kuepukana na adha ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa muda mrefu.
“Niwapongeze wananchi wa kata ya
Maweni namna walivyoweza kujitolea kushirikina na serikali yao katika
kumaliza changamoto zinazowakabili kwani hii inaonyesha kuwa ili
kuharakisha maendeleo ya sehemu husika kunahitaji ushirikishwaji wa
pande zote”alisema Mbunge Mbaruk.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata wa mtaa wa kichangani Ziada Ali alisema kuwa wakazi wa mtaa huo walilazimika kutembea umbali wa Km 5kwa ajili ya kutafuta huduma hiyo kila siku.
Alisema kuwa mradi huo utakapo
kuwa umekamilika itakuwa ni faraja kwa wananchi wa mitaa ya Jaribu tena
na Mwishi wa shamba pamoja na kuwapunguzu adha ya kwenda mwendo mrefu
kwa ajili ya kutafuta huduma ya maji.
Vile vile Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Lucas Nyengo alisema kuwa kwa takribani miaka minne wamekuwa wakiomba kupatiwa huduma hiyo lakini wanashukuru kwa awamu hii kupatiwa mradi huo.
Alisema kuwa kufuatia shida ya maji ilidumu kwa muda mrefu waliamuakuunga mkono jitihada za mamlaka kwa kushiriki katika uchimbaji wa mtaro ili kuharakisha mradi huo.
Alisema kuwa kutokana na shida ya maji iliyokuwa inawakabili
walilazimika kununua ndoo moja kwa kiasi cha sh 500 jambo ambalo ni gharama kubwa ukilinganisha na uhitaji wa huduma hiyo
walilazimika kununua ndoo moja kwa kiasi cha sh 500 jambo ambalo ni gharama kubwa ukilinganisha na uhitaji wa huduma hiyo
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment