Mkuu wa
wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akiwa katika ziara ya kuzitembelea shule za msingi za kata ya Bomalang'ombe na kujionea jinsi gani shule hizo zinavyoongozwa na kuzitambua changamoto zinazowakabili walimu,wanafunzi,wanachi na viongozi wanaozizunguka shule hizo lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wa wilaya ya kilolo.
Mkuu wa
wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bomalang'ombe.
Na Fredy Mgunda,Iringa
Wanachi wa kijiji cha
mwatasi wamekuwa kikwazo cha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya shule ya
msingi kutokana na wazazi kutowatimizia mahitaji muhimu watoto wao pindi
waendepo shule.
Akizungumza na waandishi wa
habari waliofika katika shule hiyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi mwatasi Seth
Mfikwa alisema kuwa wazazi wengi wa kijiji hicho wamekuwa kikwazo cha maendeleo
ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.
“Hapa kijijini wazazi wengi
hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao
mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi
kusoma kwa uhuru” alisema Mfikwa
Mfikwa alimuomba mkuu wa
wilaya ya kilolo Asia Abdallah kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa
elimu wazazi wa kijiji cha Mwatasi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kijiji
hicho.
“Ukiangalia hali ya ufaulu
wa shule hii sio mzuri kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu lakini
tunaendelea kuwaelimisha kidogo kidogo hivyo kwa kuwa mkuu leo umefika kwenye
shule yetu tunaomba msaada wako wa kutoa elimu kwa wazazi ili kukuza elimu kwa
wanafunzi wa kijiji hiki” alisema Mfikwa.
Aidha Mfikwa alisema kuwa
wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo
jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kijiji
hichi wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu.
Anderson Mdeke ni diwani wa
kata ya Bomalang’ombe alikiri kuwa wazazi wa kijiji cha mwatasi hawana elimu
juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na
taifa kwa ujumla.
“Kweli kabisa wazazi wa
kijiji cha mwatasi wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili
wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo
wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na dio furaha kwa wazazi wa kijiji
cha Mwatasi” alisema Mdeke
Mdeke alisema kuwa uongozi
wa kata ya bomalang’ombe utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali
ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la
kuboresha maisha ya watoto hao.
“Zana potofu zimekuwa
kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kijiji cha Mwatasi hivyo
tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Mdeke
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliahidi kulifanyia kazi tatizo hilo kwa
kuzungumza na wazazi ili kuwaelimisha juu ya umuhimu wa elimu kwa wananchi wa
kijiji hiki cha Mwatasi.
“Tangu nianza ziara katika
wilaya ya kilolo leo ndio nimekutana nah ii changamoto ya wazazi kuwarudisha
nyuma kielimu hivyo nitatenga muda muafaka wa kuja kuongea na wazazi wa kijiji
cha Mwatasi kwanza swala hili limenishtua sana kwakweli lazima nilitafutee
ufumbuzi haraka sana”alisema Abdallah
Aidha mkuu wa wilaya hiyo
Asia alisema anatakiwa kujifunza tabia za wananchi wa kijiji cha Mwatasi
kwanini wanafanya hivyo kwa kuwa changamoto hiyo ni kubwa na inatakiwa
kutatuliwa mapema.
“Unajua lazima nijue chanzo
cha kuwakatisha tamaa watoto wao wasiendelee na masomo ni nini hivyo nikijua
tatizo ni nini naweza kutatua tatizo hilo kwa urahisi kabisa maana elimu ni
kitu mhimu sana kwa maendeleo ya watoto yao” alisema Abdallah
Abdallah alisema licha ya
changamoto hiyo ya wazazi hata walimu wa shule wanamatatizo kwani haiwezekani
kuwa na walimu wengi hivi lakini ufaulu bado upo chini lazima kukaa chini na
hawa walimu kujua tatizo ni nini.
No comments:
Post a Comment