Mama nguli wa mitindo Asya Idarous Khamsin hataweza kuwepo au kufanya onyesho la mavazi leo siku ya Ijumaa kutokana na kukwama kutokana na mvua kubwa zilizonyesha Houston na kusababisha mafuriko makubwa.
Aidha Mama mitindo amewaomba radhi mashabiki na wadau wote wa mitindo watakaofika Columbus leo kwenye Bash la Old School Reunion na wengine wakiwa na shauku ya kumwona. Kutokana na sababu ya mafuriko Houston ameshindwa kushiriki kwenye Mnuso huu mkongwe na wa kihistoria kuliko yote nchini Marekani.
Pia mwanamitindo huyo nguli wa kimataifa Asya Idarous Khamsini amemtakia kila la kheri mwanamtindo Missy Temeke kwenye onyesho la mavazi litakalo fanyika leo ijumaa Sept mosi siku ya kwanza ya OLD SCHOOL REUNION na kuwatakia wadau na mashabiki wote wa old school reunion BASH JEMA la kula bata, burudani, fashion show na michezo kwa siku tatu
Missy T yeye yupo tayari Columbus tangia siku ya alhamis jioni Aug 31 na yupo tayari kubeba mikoba yote katika kufanya show kali itakayokua historia ya OLD SCHOOL REUNION
No comments:
Post a Comment