Friday, September 1, 2017

Video: Uganda wainyuka Misri, Okwi atupia goli la dhahabu

Okwi akishangilia baada ya kutupia goli la ushindi dhidi ya Misri.
Jana mashabiki wa soka duniani hususani wanaofuatilia mpira wa bara la Afrika walishangazwa na kiwango cha soka kilichoonesha na timu ya taifa ya Uganda kwa kuichapa Misri goli 1-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa wenye ushindani zaidi kutokana na timu hizo kupigana vikumbo kwenye nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo wa kundi E linaloundwa na timu za taifa za Ghana na Congo.
Goli hilo la kipekee limepatikana kupitia kwa mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi kunako dakika ya 52 ya kipindi cha kwanza.
Timu ya Taifa ya Uganda inaendelea kuweka rekodi ya kutopoteza mchezo wa kufuzu kombe la dunia wakiwa nyumbani tangia mwaka 2004 walivyopoteza dhidi ya Bafana Bafana
Kwenye msimamo wa kundi E kwa sasa Uganda wanaongoza kwa pointi 7 wakifuatiwa na Misri pointi 6, Ghana pointi 1 na Congo wakishika mkia kwa alama 0.
Mechi za kufuzu kombe la dunia 2018 zitaendelea leo ambapo Nigeria watavaana na Cameron, Tunisia vs DR Congo, Morocco vs Mali, Cape Verde vs Afrika Kusini na Ghana watavaana na Congo.

No comments: