ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 20, 2017

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AELEKEA MKOANI ARUSHA KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya Kikazi. PICHA NA IKULU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 20 Septemba, 2017 ameondoka jijini Dar Es salaam kuelekea mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA,Rais Dkt. Magufuli ataanza ziara yake Mkoani Manyara kwa kufungua barabara ya Kia - Mererani yenye urefu wa kilomita 26, na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.

Tarehe 23 Septemba 2017, Rais Dkt. Magufuli atatunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es salaam , Rais Dkt. Magufuli ameagwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar Es Slaam. 20 Septemba 2017.  

No comments: