ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 30, 2017

TANZANIA DMV KUCHEZA NA VITAMBI FC LEO JUMAMOSI SEPT 30, 2017 HEURICH STADIUM HYATTSVILLE

Image result for timu ya tanzania dmv
Timu ya Tanzania
Image result for timu ya tanzania dmv
Timu ya Vitambi


Timu ya soka inayoundwa na Watanzania DMV leo Jumamosi Sept 30, 2017 saa 11:30 jioni itacheza mechi ya kirafiki na timu ya Viambi FC inayoundwa na Wakenya waishio DMV katika kiwanja cha Heurich kilichopo Hyattsville, Maryland, mechi inatarajiwa kuwa kali na ya kusisimua.

Timu hizo zilipokutana Tanzania waliibuka na ushindi wa bao 3-2 ushindi ambao timu hiyo ya Vitambi iliulalamikia kwamba mwamuzi alipendelea upande mmoja.

Timu ya Tanzania DMV inayobeba jina la Ngorongoro Crater wameahidi kufanya kweli mechi ya leo inayosubiliwa sana na mashabiki wa soka DMV na vitongoji vyake.

Timu ya Vitambi inataka kutumia mchezo huo kwa kujaribu wachezaji wao wapya na pia kulipiza kisasi na wameahidi kuifunga timu ya Tanzania DMV kwani wamedai timu yao ipo vizuri sana mwaka huu kuliko miaka yote nyuma.

Mara nyingi timu hizi zinapokutana mechi inakua kali sana na huwezi kutabili mshindi. Kutoka timu ya Tanzania DMV wao wameahidi ushindi mnono na wamewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi na mapema kwani biashara asubuhi.

Anuani na jina la uwanja ni  Heurich Stadium 2800 Nicholson street Hyattsville MD.

Msemaji wa timu ya Tanzania amewataka wachezaji wanakaotaka kucheza mechi hiyo wawasiliane mapema kupitia 202 790 2742 na ameomba atakayekuwepo  aje na $10 ya kusaidia kulipia uwanja na amesisitiza kufika uwanjani dakika 30 mapema. Karibuni

No comments: