Mvurugano huo umeonekana leo Jumatatu mjini Dodoma baada ya wabunge wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma kuwa mwenyekiti wao bungeni.
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametangaza kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amepokea barua kutoka kwa Katibu wa CUF, Magdalena Sakaya kuhusu safu hiyo ya uongozi.
Baada ya tangazo hilo, Mbunge wa Malindi, Ally Salehe aliomba mwongozo wa Spika akitaka kujua ni nani anaamua kuhusu uongozi wa wabunge bungeni kwa sababu wao wameshafanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kuwa mwenyekiti wao baada ya kufukuzwa kwa wabunge wanane.
Akijibu mwongozo huo, Dk Tulia amesema Spika amepokea taarifa ya viongozi hao lakini hajapokea taarifa ya uchaguzi wa upande wa akina Ally Salehe ambao unamuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Amesema watakapopeleka taarifa yao ndipo Spika ataamua.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment