Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira alilithibitishia HabariLeo jana kuwa watu hao walimvamia Ofisa Tarafa huyo nyumbani kwake muda wa saa tatu na nusu usiku na kumshambulia kwa kitu chenye ncha kali na kupoteza maisha.
“Ofisa Tarafa alikuwa amekaa sebuleni kwake ambapo watu hao wasiofahamika walimvamia na kuanza kumshambulia kwa kitu chenye ncha kali na kumuua na kisha kutokomea,” alieleza Kaimu Kamanda Rwegasira.
Kwa mujibu wa Rwegasira, chanzo cha mauaji hayo hakijulikani na hakuna mtu anayeshikiliwa mpaka sasa. Alisema upelelezi unaendelea ili kubaini chanzo na wahusika. Aliongeza kuwa Ofisa Tarafa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 58, alikuwa akiishi pekeyake kwenye nyumba hiyo.
Tarafa ya Lupiro wilayani Ulanga inakabiliwa na ongezeko la watu kutokana na kuwa maarufu kwa kilimo cha mpunga na biashara ya mchele, lakini pia tarafa hiyo iko njiapanda ya kwenda Makao Makuu ya Wilaya ya Ulanga-Mahenge na Wilaya ya Malinyi.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment