Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe (katikati) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki wa wakala huo kabla ya kuwatunuku vyeti baada ya kumaliza mafunzo hayo. Kulia ni Mhandisi Aurelia Ngopa na kushoto ni mkuu wa chuo hicho Mhandis Lucius Luteganya. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
Mkuu wa chuo cha VETA Kipawa ICTC Mhandisi Lucius Luteganya (wa pili kushoto aliyesimama) akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) waliofuzu mafunzo hayo katika zoezi la kuwatunuku vyeti lililoandaliwa na Kituo hicho. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wakisubiri kukabidhiwa vyeti vyao mara baada ya kumaliza mafunzo hayo katika chuo cha VETA Kipawa ICTC. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe akimkabidhi cheti cha kuhitimu mfanyakazi wa wakala huo Jane Wilson Sawala mara baada ya kuhitimu mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki katika chuo cha VETA Kipawa ICTC. Wa kwanza kulia anayetazama ni Mhandisi Aurelia Ngopa. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
Wahitimu waliofuzu mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki katika chuo cha VETA Kipawa ICTC wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe (katikati aliyekaa) mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao baada ya kumaliza mafunzo hayo. Kulia aliyekaa ni Mkuu wa chuo hicho Mhandisi Lucius Luteganya na kushoto ni Mhandisi Aurelia Ngopa. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika kituo hicho kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam na yalihusisha jumla ya watumishi 15 wa TEMESA.
Na Alfred Mgweno, TEMESA
Jumla ya watumishi 15 kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jana (Septemba 19, 2017) wamehitimu mafunzo ya TEHAMA na Elektroniki kutoka katika Chuo cha TEHAMA VETA (Kipawa Information and Communication Technology Center) kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yalihusisha watumishi kutoka mikoa ya Dodoma, Kigoma, Njombe pamoja na Dar es Salaam.
Akizungumza katika sherehe za Mahafali hayo, Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe , alitoa wito kwa wahitimu hao kuhakikisha wanautumia ujuzi walioupata chuoni hapo kuundeleza wakala kutoa huduma kwa ufanisi mkubwa unaoendana na mabadiliko ya kiteknolojia na pia kuwa mabalozi wazuri popote watakapokwenda
“Lengo la kuwaleta kwenye mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa mnaendana na mabadiliko ya teknolojia inayobadilika kila wakati na pia kuwafanya muwe wabunifu wa mifumo mipya kila inapotokea”
Aidha, Mhandisi Simfukwe, alimshukuru Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Lucius Luteganya kwa mapokezi mazuri aliyowapatia watumishi wa wakala pamoja na kukubali kuwapa mafunzo hayo pamoja na wakufunzi kwa ushirikiano waliouonyesha kwa wahitimu hao, pia aliwahimiza waendelee kutoa mafunzo kwa weledi na ubunifu,kwa Watanzania wanaofanya nao kazi, ili kuongeza wajuzi wa fani hizo za TEHAMA.
Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Mhandisi Lucius Luteganya, alitoa historia ya Kipawa ICTC, na kusema kuwa, Serikali iliamua kuwekeza katika Kituo hicho kwa malengo ya kutoa mafunzo ya TEHAMA na kukifanya chuo hicho kua kisima cha taaluma na ujuzi hapa nchini.
Mafunzo hayo yalihusisha Usambazaji wa mifumo ya nyaya, Uunganishaji wa nyaya za kubebea mifumo ya TEHAMA, Mpangilio wa vifaa vya kielektroniki vya kuzuia uingiaji kwenye jengo, Kamera za ulinzi, Mifumo ya mawasiliano isiyotumia nyaya, Mfumo wa mahudhurio wa kielektroniki, Mfumo wa mawasiliano ya kitoa nakala, Viashiria vya moto pamoja na Vizimia moto.
No comments:
Post a Comment