Naibu Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (FATAH) Dkt. Uriel Davis, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za makusudi kumaliza ‘Ukaburu’ pekee uliobakia duniani unaofanywa na Israel dhidi ya Palestina,ambayo pamoja na kuikalia kimabavu pia inaendesha ubaguzi wa rangi na kitaifa, sawa na ule uliowahi kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Dkt.”Uriel Davis”ametoa wito huo katika salamu zake kwenye hafla ya chakula cha usiku, iliyofanyika Jumanne wiki hii Oktoba 3 katika hoteli ya “Double Tree Hilton” jijini Dar es Salaam, ambayo imeandaliwa na Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe. “Hazem Shabat” na kuhudhuriwa na waandishi wa habari,wataalamu na wanaharakati mbalimbali.
Aidha ameongeza kusema: ”Israel remains the only apartheid state that is a member state in the United Nations”, akimaanisha kuwa Israeli imebakia taifa pekee la ‘kikaburu’ ambalo ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa, linaloendelea kuwakalia wapalestina kimabavu,kuwabagua na kuwapora haki zao za kibinaadamu. Huku akitoa wito kwa walimwengu kuungana pamoja katika kupigania ukombozi wa Palestina,ikiwa ni pamoja kuchukua hatua ya kuisusia kibiashara,kiuchumi na kisiasa,jambo ambalo analiweza hata mtu wa kawaida.
Akifafanua na kutoa mifano ya ‘ukaburu’huo ujulikanao kama “racism/apartheid”,amesema umekuwa ukiungwa mkono na sheria pia kanuni zinazowekwa na bunge la nchi hiyo dhalimu ya Israel, ambayo awali ilivamia Palestina na kuendesha harakati za ‘usafishaji’wazawa wenye ardhi,zoezi lijulikanalo kama “Ethnic cleansing of the indigenous people of Palestine”. Huku akikumbusha zama za ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya kusini, ambapo asilimia 87 ya ardhi ilikuwa kwa matumizi ya weupe pekee kisheria, hivyo hivyo leo Palestina ukiacha Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, asilimia 93 ya ardhi ni kwa matumizi ya wayahudi (Jews) pekee.
Kwa upande mwingine,amevitaka vyama vya kisiasa kusimamia serikali zao na kuzielekeza malengo yao ya ukombozi zisusie taifa hilo kidiplomasia,akigusia hivi sasa Israel inapigania kupata kiti cha mjumbe mtazamaji “Observer status” katika umoja wa Afrika. Hivyo, itakuwa kosa kubwa kuikubalia hilo hasa ukizingatia nchi nyingi za Afrika zilipinga vikali Ubaguzi nchini Afrika ya kusini.
Dkt.Uriel Davis ametoa tahadhari hiyo,kufuatia harakati za Waziri Mkuu wa Israel “Benjamin Netanyahu”kutaka nchi yake kupewa kiti katika Umoja huo wa Afrika “AU”, alipozuru baadhi ya nchi za Afrika mwezi Julai mwaka jana 2016, huku Palestina ikiwa tayari ni mwanachama msikilizaji katika “AU” kwa muda mrefu sasa.
Mbali na Tanzania, Dkt. “Uriel Davis” pia atatembelea nchi za Afrika ya Kusini,Msumbiji,Zambia,Senegal na Ethiopia, akiwa na lengo la kuongea na vyama tawala vya nchi hizo kuviomba kuzishinikiza serikali zaokususia pia mpango ujulikanao kama “Togo initiative”, ambao tayari Israel inaonekana kutia mguu.
Dkt. “Uriel Davis” ni Myahudi aliyezaliwa mjini Jerusalem mwaka 1943, lakini amekuwa mpinzani mkubwa wa siasa za Kizayuni “Zionism”,hupenda kujiita “A Palestinian Hebrew national of Jewish origin,anti-Zionist”. Baada ya kusilimu na kuoa mwanamke wa kipalestina,ameongeza wasifu wake na kujiita: “A Palestinian Hebrew national of Jewish origin,anti-Zionist,registered as Muslim and a citizen of an apartheid state – the State of Israel”. Harakati zake zimempelekea kuwa muungaji mkono mkubwa wa harakati za Wapalestina katika kupigania uhuru na haki zao,akianzia ndani ya chama cha kupigania haki za kiraia “Israeli League for Human and Civil Rights”.
Akiwa kama msomi na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bradford,alisomesha somo la Amani “Peace Studies”,ni mwanachama wa Chama cha FATAH toka mwaka 1984 na mwaka 2009 akachaguliwa kuingia katika Baraza la Uongozi la Chama cha Wapalestina “Fataha’s Revolutionary Council”, lenye wajumbe 128 na kuwa mjumbe wa mwanzo mwenye asili ya kiyahudi “Jewish” kuingia humo,huku akichaguliwa tena nafasi hiyo mwaka 2016.
Vilevile ni mwanzilishi wa harakati za kupinga ukandamizaji na ubaguzi dhidi ya Wapalestina zijulikanazo kwa jina la “The Movement Against Israeli Apartheid in Palestine - MAIAP” na “Al-Beit The Association for the Defense of Human Rights” katika Israel. Mnamo mwaka 2008 alisilimu na kuoa Mpalestina Bi.Miyassar Abu Ali, ambae japo ni mke halali lakini haruhusiwi kukanyaga Jerusalem nyumbani kwa mumewe kutokana na vikwazo vya ubaguzi haramu wa Israeli.
Ubaguzi huo,umemfanya abaki mjini Ramallah kwa mkewe na akitaka kuwatembelea ndugu zake basi huenda bila ya mke,isipokuwa anasema anapata faraja kuungana na mkewe huyo katika kupigania haki za Wapalestina. Aidha ametoa wito kuwa,watu wasikubali kutukanwa ovyo,kuvunjiwa heshima zao na kupewa majina mabaya, endapo ikitokea hivyo afungue kesi mahakamani kudai fidia na kusafishwa.
Dkt.”Uriel Davis”amemalizia salamu zake kwa kutoa wito huo,kufuatia hatua ya Israel ya kuwaandama wanaopinga ubaguzi wake, kwa kuwapa majina mabaya kama gaidi na ‘antisemite’,kwa maana ya kutaka Israel isiwepo au iangamizwe kwa Uyahudi au Uisraeli wake, kwa kufanya hivyo Israel kana kwamba inatumia mbinu ya kuficha ubaya wake. Israeli haipingwi kama yeye pia “Jew” haipingwi kama “Jew”, bali kinachopingwa ni ubaguzi na ukandamizaji wake dhidi ya Palestina.
No comments:
Post a Comment