ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 7, 2017

HOSPITALI YA RABININSIA MEMORIAL YAPEWA HATI YA KUTHAMINIWA NA BENKI YA AZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(kushoto) akimsiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe alipokuwa anazungunza kuhusu namna benki ya Azania inavyowajali wateja wao wadogo wadogo, wa kati na wakubwa na kwenda nao bega kwa bega ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea pamoja nakueleza bidhaa walizonazo katika benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema akizungumza kuhusu changamoto na faida anazozipata kupitia benki ya Azania pamoja na kushauri namna nzuri kuwajali wateja wao mara alipotembelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) ofisini kwake.
  Meneja wa benki ya Azania tawi la Tegeta, Geofrey S. Mahona(kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati wakifuatilia mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema alipokuwa akisisitiza jambo kuhusu benki ya Azania.

Mkutano ukiendelea wakati wakati wa maofisa wa benki ya Azania pamoja na Mkurugenzi wao walipomtembelea mteja wao ofisini kwake kwa ajili ya kutaka kujua ni changamoto zipi anazipata kwenye biashiara yake. Kushoto ni uongozi wa Hospitali hiyo na kulia ni viongozi wa benki ya Azania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) akimkabidhi hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(wa pili kutoka kushoto).
Picha ya Pamoja

Na Mwandishi Wetu

Benki ya Azania imeendelea kutembelea Wateja wake katika Wiki ya Huduma kwa Wateja baada yakufika katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Hospitalini hapo,  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe ameishukuru Hospitali hiyo kwa kuwa Wateja Wakubwa wa Benki hiyo.


Itembe amesema kuwa Wiki hiyo ya Huduma kwa Wateja ni muhimu sana kwa kuwa Benki inatambua mchango wa Wateja wake katika kutoa huduma. Pamoja na kuomba uongozi wa hospitali hiyo kutumia bidhaa nyingi za benki hiyo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Elisania Lema ameishukuru benki hiyo ya Azania kutambua mchango wa Hospitali hiyo kwa kuwa wanafarijika wakiona wanatembelea mara kwa mara na Uongozi wa Benki ya Azania. 



Hata hivyo, Dkt. Lema ameiomba Benki hiyo kutambua na kujali Wateja wake pindi wanapofika katika Matawi yake ili kuondoa usumbufu pale wanapotaka kupata huduma .

No comments: