Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi
wanawake mkoani Iringa (TPF)
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi na mbunge wa viti maalum mkoani
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi
wanawake mkoani Iringa (TPF)
Hawa ni baadhi ya wanamtandao wa polisi
wanawake mkoani Iringa (TPF) wakiwa katika maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa kwa mwaka 2007.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoani
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alikuwa mgeni rasmi
katika maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi
wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa lengo la kufanya kazi kwa ukaribu na jamii.
Akisoma risala iliyoandaliwa
na mtandao huo PC Doroth Matinde alisema kuwa mtandao wa polisi wanawake Tanzania
(TPF) ulianzishwa mnamo tarehe 25 / 10 / 2007 kwa lengo la kuendelea kuifnya
kazi kwa karibu kwa jamii na kufanikisha azma ya utekelezaji wa majukumu yake.
“Lakini ukiangalia na yote
hayo lengo na malengo mengine ni kuunganisha askari wa kike kuwa karibu na
jamii ili kudumisha mahusiano mema kati ya mtandao na wananchi hatimaye
kuboresha huduma bora na kufanikisha ufanyaji kazi wetu” alisema Mtinde
Mtinde alisema kuwa mtandao
huo wa polisi wanawake umekuwa ukitembelea akina mama wajane,kuwafariji na kuwapa
msaada wa chakula ndani ya kambi za polisi hapa mkoani Iringa.
“Katika kuhakikisha kuwa
mtandao unathamini nafasi ya mwanamke katika jamii tumekuwa mstari wa mbele
kushirikiana kwa kutoa elimu ya masuala kadha kama ubakaji,ulawiti,Imani potofu
na unyanyasaji wa kijinsia” alisema Mtinde
Aidha Mtinde alizitaja kazi
watakazozifanya kazi katika cha maanzimisho
watafanya usafi katika maeneo ya soko kuu manispaa ya Iringa,stendi kuu
pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi mbalimbali wa shule za msingi na sekondari
ili kuzuia uhalifu na kutoa elimu ya madhara ya madawa ya kulevya na mimba za
mashuleni.
Kwa upande wake mgeni rasmi
Ritta Kabati aliupongeza mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa
kufikisha miaka kumi ya kuwatumikia wananchi na kuhakikisha wazitatua
changamoto zilizowakabili wananchi na kuifanya jamii kuendelea kuishi kwa Amani.
“Kwa kweli naona wanamtandao
mnajitahidi sana kufanya kazi na kazi yenu inaonekana katika jamii hasa
kuanzisha hata dawati la jinsi hapa mkoani Iringa limekuwa jambo la muhimu sana
kwa wanawake” alisema Kabati
Kabati aliwachangia shilingi
milioni moja kwa ajili ya kufanikisha shughli za mtandao wa polisi wanawake mkoani
Iringa (TPF) na kuhaikisha anawatafutia wafadhi wa kusaidia kutatua changamoto
ili kuifikia jamii kwa urahisi Zaidi.
“Mimi natoa hiki kidogo tu
lakini nitahakikisha nawatafuta wafadhili wengine ili kuendelea kuuchangania
mfuko wa huu mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa ajili kuweza
kuifikia jamii na kufanikiwa kutatua changamoto kwa haraka Zaidi” alisema
Kabati
Kabati aliliomba jeshi la
polisi mkoani Iringa kuhakikisha wanapeleka dawati la jinsia katika shule za
msingi na sekondari ili kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi
kwa kuwa watakuwa wazi kuzungumza wanachofanyiwa huko mitaani.
“Tukiwa na madawati katika
shule zetu itasaidia kupunguza tatizo la ubakaji kwa wanafunzi wetu hivyo
kamanda naomba mtafute njia ya kuweza kufanikisha kuwa na madawati ya jinsia
kama ambavyo PCCB walivyoenea katika shule mbalimbali” alisema Kabati
Naye kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa Julias Mjengi alisema kuwa jeshi la polisi hapa nchini lipo katika hatua
za mwisho za kukamilisha mpango wa kulipeka dwati la jinsia kwenye shule za sekondari
na shule za msingi kwa lengo lakuanza kutoa elimu mapema za ukatili wa kijisia.
“Ulicho kiongea mgeni rasmi
ni kweli tatizo lipo sana mashuleni hivyo tuanza mikakati ya kuahikisha
tunawafikia wanafunzi katika ngazi zote” alisema Mjengi
Mjengi alimpongeza mbunge
Ritta kabati kwa juhudi zake za kulisaidia jeshi la polisi mkoani Iringa kwa
hali na mali kwa kuwa amekuwa mstali wa mbele kutatua changamoto za jeshi hilo.
“Najua kuwa ulijenga kituo
cha polisi kule semtema,umetoa kompyuta na mambomengine mengi ambayo jeshi la
polisi tulikuwa hatuna uwezo kuyatekeleza kwa urahisi kama ambavyo kabati
amefanikiwa kuyatatua” alisema Mjengi
No comments:
Post a Comment