Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Vijijini ikijihuzuru mbele ya wajumbe muda mchache kabla ya mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Singida Vijijini.
Msimamizi wa uchaguzi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Singida Vijijini.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.
Wajumbe wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Singida Vijijini wakifatilia kwa makini mkutano wa uchaguzi.
Na
Mathias canal, Singida
Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.
Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya
Ilongelo na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM
Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.
Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni
aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni William Mwang'ima Nyalandu aliyepata
kura 440, akifatiwa na FATUMA Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu
ilikamatwa na Alex Mdidi Lissu aliyepata kura 159.
Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema
kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata taratibu na
kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.
Alisema kuwa pamoja na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa
CCM Wilaya lakini pia nafasi zingine zilizowaniwa ilikuwa ni pamoja na Nafasi
Ya Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ambapo Richard Niangusha Kwimba aliibuka
mshindi kwa kupata kura 6, nafasi ya
pili ni Khamisi Swalehe Kimu kura 35, Iddi Athumani
Monko kura 8 na Swalehe Munkumbu Sungi
aliyepata kura 3.
Nafasi ya Halmashauri Kuu ya Wilaya waliogombea ni 27 ambapo kati yao walioshinda ni Sabasaba Manase, Edward Jared Ihondo, Japhet Ntandu Gham, Justin Joseph Monko, Mohamed Abdallah Ghamayu, Nkumbi Mohamed Kemi, Zuena Dunya, Simon Mumbai, Shabani Ally Mang'ola, na Wiliamu Mwang'imba Nyaland.
Nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliomba walikuwa watano lakini washindi kati yao ni Mchungaji Wilson Mtatuu Ihucha, na Sada Njiku. Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoa ni Sabasaba Manase, Shaban Mang'old na Edward Jared Ihonde.
Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Singida Bi Grace Shindika alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya wananchama na viongozi wote waliochaguliwa ili kuongeza ufanisi na nguvu ya chama katika Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
MWISHO
No comments:
Post a Comment