Mwenyekiti wa serikali ya mtaa
wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden
Madembo akiwa na mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kuzitambua changamoto zinazoikabili shule ya msingi Igeleke iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa
wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden
Madembo akiwa na mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakiwa katika picha nawanafunzi wa darasa la saba
Mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua madarasa ambayo miundombinu yake imeharibika.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa
wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden
Madembo amempigia magoti mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati
kuwasaidia kukarabati shule ya msingi Igeleke kwa kuwa miundo mbinu yake
imeharibika na sio rafiki kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Akizungumza na blog bwana
Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi
wa shule hii kwanza toka mwaka 1978 hadi leo shule hiyo haijawahi kufanyiwa
ukarabati wa kueleweka hivyo inahitajika kukarabatiwa haraka iwezekanavyo.
“Mwandishi ukiangalia
majengo ya shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo katika halmashauri
ya manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi hawaingalii kwa jicho la tatu kitu
kinachotupa shida sisi viongozi wa eneo hili” alisema Madembo
Madembo alisema kuwa shule
nyingi zilizojengwa miaka ya 1978 na kuendelea zinamiundombinu ilichoka hivyo
serikali na viongozi wa kisiasa kuanza kuzitafutia mikakati ya kuzikarabati ili
kuboresha taaluma kwa watoto wetu kuendana na karne ya sasa.
“Hebu angalia hapo juu hili
paa muda wowote kuanzia sasa hili paa la darasa linaweza kuleta maafa kwa
wanafunzi lakini viongozi wetu hawaliangalii hili swala ndio maana nimemuaomba
huyu mbunge Ritta Kabati kusaidia kuarabati” alisema Madembo
Aidha Madembo alisema kuwa
haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi waliotayari kule maendeleo
kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua
wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.
“Leo hii mimi ni mwenyekiti
wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta
maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi
kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo” alisema Madembo
Kwa upande wake mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati
alisema kuwa anafanyakazi na wenyeviti wote wa manispaa ya Iringa kwa lengo la
kuijenga manispaa na kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Iringa.
“Nimekuwa navikao vya mara
kwa mara kwa wenyeviti wa mitaa ya hapa manispaa hivyo wenyeviti wa CHADEMA
wamekuwa wa kwanza kuniita kila wakati kusaidia kuleta maendeleo katika maeneo
husika ndio maana leo unaniona nipo na mwenyekiti wa CHADEMA kutafuta njia
mbadala ya kutatua changamoto za hii shule ya Igeleke” alisema Kabati
Kabati aliwataka viongozi
mbalimbali kutafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo wananchi nsio kuangalia
vyama vinafanya nini.
“Mimi ni kada wa chama cha
mapinduzi lakini nimekuwa nikifanya kazi vizuri na viongozi mbalimbali wa kiasa
kwa lengo la kuleta maendeleo tu ndio sababu inayosababishwa wapinzani kuniona
mimi bora wakati wa kufanya shughuri za kuleta maendeleo” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa
ataendelea kufanya ziara kwenye shule zote zenye matatizo ili kuzisaidia
kuyatatua matatizo hayo na leo amefanya ziara katika shule ya
msingi Igeleke kwa kuziona changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuzitafutia ufumbuzi.
Naye mkuu wa shule ya msingi
Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru
mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya
shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
No comments:
Post a Comment