ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 19, 2017

TRUMARK WAPATA MAFUNZO YA KUBORESHA UFANISI TOKA SHIRIKA LA PUM KUTOKA NCHI YA NETHERLANDS

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akimshukuru Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka  nchi ya Netherlands,  Paulus Joseph Maria Jaspers wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam
 Washiriki wa mafunzo hayo kutoka Trumark wakiwa katika majadiliano. Kutoka kulia ni Meneja wa Idara ya Biashara na Masoko wa Kampuni hiyo, Grace Sikazwe, Mratibu wa Miradi, Gwamaka Mwakijengele na  Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini, Ismail Omcoi.
 Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka  nchi ya Netherlands,  Paulus Joseph Maria Jaspers akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo wakati wa mafunzo hayo. Wengine ni maofisa wa kampuni ya Trumark.
Maofisa wa Kampuni ya Trumark wakiwa kwenye mafunzo hayo. Kutoka kulia ni MaryRose Mphuru, Adam Musoni na Msusa Geuzye.


Picha ya pamoja.

 Mkufunzi akipongezwa.
 Mtaalamu wa Idara ya picha wa kampuni hiyo, Juma Diwani akiwa kwenye mafunzo hayo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Trumark imepata mafunzo ya kuboresha ufanisi wa kazi kutoka Shirika la PUM-Netherlands Senior Exparts.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwakilishi wa Shirika hilo, Deogratias Mbona alisema mafunzo hayo yanatoa fursa kwa walengwa kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo biashara.

"Mafunzo haya yanatolewa katika nchi 31 duniani na yameweza kuyanufaisha makundi mbalimbali ya jamii hasa vijana" alisema Mbona.

Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa kujitolea na yamelenga kuwawezesha vijana katika biashara, kilimo, uzalishaji viwandani na utoaji wa maarifa kutoka kwa wakufunzi wa shirika hilo waliobobea katika masuala hayo.

Kwa Kampuni ya Trumark ambayo imetoa maofisa wake 10 kushirika mafunzo hayo wao watanufaika na uboreshaji wa miradi na kupanua masoko pamoja na kukutanishwa na wadau wengine wa mataifa mbalimbali na kubadilishana nao uzoefu.

No comments: