Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Mteja wa PSPF, ambaye ni Mstaafu, Bw. Kassim Salehe Mafanya, (63), wakifurahia jambo wakati kiongozi huyo wa alipomtembelea Mstaafu Mafanya nyumbani kwake Kitunda B, nje kidogo ya jiji Oktoba 4, 2017 wakati Dunia ikiadhimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja.
Bw. Mafanya, (kulia), akipokea fomu hiyo |
Wakati
Wiki ya Huduma kwa Wateja ikiendelea kote Duniani, Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
umeitumia wiki hiyo sio tu kwa kuhudumia wateja ofisini bali pia kutoka nje ya
ofisi na kuwatembelea Wanachama na Wastaafu wa Mfuko huo majumbani kwao.
Mmoja
wa waiotembelewa ni Mstaafu Bw. Kassim Salehe Mafanya,(63), anayeishi Kipunguni
B, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kitendo ambacho kilimfurahisha sana.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu, wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa akifuatana na timu yake, Oktoba 4,
2017 alifika nyumbani kwa Bw. Mafanya, na kufanya mazungumzo naye ikiwa ni
pamoja na kumpatia fomu ili aijaze kwa nia ya kumuhakiki kama ambavyo sheria
inataka.
Kwa
mujibu wa Sheria, Mstaafu anatakia kufika kwenye ofisi za PSPF kuhakikiwa kila
mwaka ili kujua uwepo wake, anasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew
Mkangaa
“Kama
mnavyofahamu wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja Duniani kote, na sisi PSPF
kupitia ofisi zetu nchi nzima tunajitoa na kutembelea wateja wetu ambao ni
pamoja na wanachama na wastaafu, na leo tuko hapa eneo la Kipunguni B, tumekuja
kumtembelea Bw. Kassim Salehe Mafanya, ambaye ni mstaafu na lengo ni kumjulia
hali na kumuhakiki uwepo wake kama ambavyo sheria inataka.” Alisema.
Afisa
Uendeshaji wa PSPF ambaye pia alifuatana na Bw. Mkangaa, alimsomea Mstaafu
huyo, maelezo yaliyomo kwenye fomu ya uhakiki kabla hajaweka saini kenyefomu
hiyo.
Aidha
kwa upande wake, Mstaafu huyo Bw. Mafanya aliishukuru PSPF kwa kitendo hicho
cha kuwatembelea wateja wao yeye akiemo na kwamba ni kitendo kinachofaa
kupongezwa.
“Siku
ya leo nimefarijika sana, kwanza sikutegemea kama nigepokea ugeni kama huu kutoka
PSPF wa kunitembelea mimi Mstaafu hapa nyumbani kwangu,” Alianza kwa kusema Bw.
Mafanya wakati akiwakaribishas viongozi hao wa PSPF.
“Kitendo
cha kuwakumbuka wastaafu kama sisi na kuwatembelea majumbani kwao
kimenifurahisha sana na niwapongeze kwa tabia hiyo, Alisema.
Bw.
Mafanya alimuhakikishia Kaimu Mkurugenzi Mkuu, kuwa amekuwa akipokea pensheni
yake kila mwezi na bila matatizo yoyote na amekuwa akipata ushirikiano mzuri
kutoka kwa maafisa wa PSPF kila anapokwenda kufuatilia pensheni yake.
“Nashukuru
pensheni yangu inaendelea vizuri, huu ni mwaka wa 14 tangu nistaafu, nachukua
vizuri tu pensheni ya kila mwezi na uzuri nikwamba inaboreshwa, na ndio maana
mpaka hivi sasa tunaonekana tuna afya nzuri na ninaendelea na shughuli zangu
mimi na familia yangu.” Alipongeza.
Bw. Mkangaa, (Kushoto), akipeana mikono na Bw. Mafanya baada ya kumtembela nyumbani kwake.
Bw. Mkangaa akisalimiana na familia ya Bw. Mafanya
Bw. Mkangaa akiwa amembeba mjukuuu wa Bw. Mafanya.
Bw. Mafanya (kushoto), akifurahia jambo na Afisa Uendeshaji kutoka PSPF, Bw.Ernest Massay
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, na timu yake akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafamilia wa Bw. Mafanya mbele ya nyumba yake.
No comments:
Post a Comment