ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 9, 2017

KATIBU MWENEZI CCM EDWIN BASHIR WAPINZANI ACHENI SIASA ZA MAJI TAKA

 Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru katika uchaguzi mdogo wa kumpata diwani atakayekuwa kiongozi wa kata hiyo huku CCM wakimuombea kura mgombea wao Baraka Kimata 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Kitwiru

Na Fredy Mgunda,Iringa

Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kufanya siasa safi kwa kutoa hoja za msingi wakati wanaomba kura kwa wananchi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru unaoendelea hivi sasa.
 
Akizungumza na blog hii Bashir alisema kuwa wapinzani wamekuwa wakitoa lugha za matusi kwa wananchi wakati wakiomba kura majukwaani.

“Kila wakisimama jukwaani ni matusi tu utafikiri ndio kura zenye mimi naomba watumie lugha za kistaarabu kuomba kura kwa wapiga kura kwa wananchi wa kata ya Kitwiru na kuwafanya wananchi kumchagua kiongozi wanaemtaka” alisema Bashir

Bashir alisema kukitukana chama chama mpinduzi ni kukikosea heshima kwa kuwa chama hicho kimekuwa kikifanya kampeni za kistaarabu bila kutoa maneno ya machafu kwa wapinzani na kuendelea kuwaaminisha wananchi kuwa CCM inafanya kampeni za kistaarab.

“Yaani saizi wakisimama kwenye majukwa kazi yao ni kutoa lugha chafu dhidi ya chama chetu hivyo mimi nawaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa watulivu na kuhakikisha mgombea wa chama cha mapinduzi anashinda kwa kishindo” alisema Bashir

Aidha Bashir aliwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpigia kura mgombea wa chama cha mpinduzi (CCM) ambae atawaletea maendeleo kwa kufuata na kutekeleza vilivyo ilani ya chama hicho kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayofanya.

“Huku CCM kuna mfumo ambao unawaongoza viongozi wetu na mambo mengi yanafanywa kwa kufuata utaratibu hivyo wananchi wanatakiwa kumwamini Baraka Kimata kwa maendeleo ya kata ya Kitwiru” alisema Bashir

Bashir amewataka viongozi wa CCM kutumia lugha nzuri wakati wa kuomba kura na matusi kuwaachia wapinzani na kutengeneza utofauti baina ya CCM na vyama vingine.

“Niwaombe wanakitwiru kuhakikisha tarehe ishirini na sita mwezi huu Baraka Kimata anaibuka mshindi katika uchazi huu mdogo wa kata hiyo” alisema Bashir

Lakini Bashir amewahakikishia wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) na wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa watashinda kwa kishindo kutokana na mikakati ya chama hicho ambayo ipo imara na dhabiti kwa ajili ya kushinda kata hiyo.

No comments: