Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe la Msingi ujenzi wa barabara ya juu Tazara (flyover) itagharimu kiasi cha
fedha Bilioni 100, za kitanzania mpaka kukamilika kwake. (TAZARA FLYOVER)
Tarehe 02 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe
La Msingi Mradi Wa Uboreshaji Wa Bandari Ya Dar Es
Salaam
Ujenzi,
ukarabati na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umepangwa kufanyika kwa
*miezi 30
kuanzia sasa kwa gharama ya
Shilingi Bilioni 926.2
(ambapo kati
yake Shilingi Bilioni 132 zinatolewa na Serikali ya Tanzania, Shilingi Bilioni
770 ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na Shilingi Bilioni 24 ni
Msaada kutoka Shirika la Maendeleo la Uingereza .
Tarehe 12 April 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ameweka Jiwe La Msingi Ujenzi Wa Reli Ya Kisasa Standard Gauge Kutoka Dar Hadi Morogoro
Tarehe 20 Marchi 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Flyover ya Ubungo, Ubungo utakaochukua miezi 30 kuanzia sasa hadi mwezi Septemba 2019, mradi mbao utagharimu takribani shilingi bilioni 188.71
Tarehe 24 Julai 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe la Msingi mradi wa maji kutoka ziwa Victoria – Tabora
Tarehe 23Julai 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi wa maji Nguruka, Uvinza( Mradi wa Maji wa Nguruka ambao utakamilika tarehe 31 Desemba, 2017 utagharimu Shilingi Bilioni 2.87)
Tarehe Agosti 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mwijage
wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha
Tanga Fresh maeneo ya Kange jijini Tanga
Tarehe 12 Januari 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe la Msingi
katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya
Maswa mkoani Simiyu
Tarehe 02 Machi 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli, ameweka Jiwe la Msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles)
cha Kampuni ya Goodwill Tanzania Ceramic Limited kilichopo katika Wilaya ya
Mkuranga Mkoani Pwani.
Kiwanda hicho kikubwa
Afrika Mashariki na Kati
-Ujenzi wake umegharimu
$Milioni 50
-Kitakuwa na uwezo wa
kuzalisha mita za mraba 80,000 za vigae kwa siku, kitazalisha ajira za moja kwa
moja 1,000 na ajira zisizo za moja kwa moja 2,000.
Tarehe 17 Novemaba 2017
Makamu wa rais Mh. Samia Suluhu
Hassan ameweka Jiwe la Msingi kwenye mradi mkubwa wa maji katika mji wa Nansio wilayani Ukerewe unaotekelezwa chini ya ufadhili wa benki
ya maendeleo ya Afrika pamoja na serikali ya Tanzania kwa - Gharama ya shilingi bilioni 10.9
na kuwataka wananchi wa vijiji 10 vitakavyonufaika na mradi huo kuhakikisha wanatunza na kulinda miumbombinu yake kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.
Tarehe 21Juni 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli, ameweka Jiwe la Msingi kwenye
sehemu ya kiwanda cha kutengeneza matrekta ya URSUS kilichopo Kibaha
mkoani Pwani.
Tarehe 21 October 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni 20 ya wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 ikiwa
ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi Juni mwaka huu wakati wa sherehe za
uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuo hicho.
Wakati Rais Magufuli akiweka jiwe la
msingi la mradi huo, tayari ujenzi umefikia asilimia 75 ambapo majengo 20
yaliyounganishwa kimuundo yamefikia ghorofa ya nne na ujenzi huo unaofanywa na
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30
Desemba, 2016.
Tarehe 05Agosti 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri
Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta
ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na
Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje
kidogo ya jiji la Tanga.
Tarehe 04 Oktoba 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkr John Pombe Magufuli, amemshuhudia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akifunua pazia kuashiria kuwekwa
kwa Jiwe la Msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) jijini Dar es salaam.
Mapema kabla ya
Marais wote wawili kuzungumza, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deodatus Kakoko alisema jengo hilo lina ghorofa
35, urefu wa meta 157, ukubwa wa meta za mraba 65,115 na ujenzi wake
unatarajiwa kukamilika tarehe 31 Desemba, 2016 kwa gharama ya Shilingi Bilioni
130.
Tarehe 16 Machi 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkr John Pombe Magufuli, ameweka Jiwe la Msingi Katika Ujenzi wa kituo cah kufua umeme cha KINYEREZI II Jijini Dar es Salaam.
Tarehe 02 Juni, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkr John Pombe Magufuli,
ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuokikuu cha Dar es
salaam inayojengwa katika kampasi ya
Mlimani upande wa mashariki mwa chuo.
Maktaba hiyo ya
kisasa itakapokamilika itakuwa ndio maktaba bora kuliko zote barani Afrika,
ikiwa na ukubwa wa eneo la meta za mraba 20,000 na itakuwa na uwezo wa kuwa na
vitabu 800,000 na kuchukua wanafunzi 2,600 kwa mpigo.
Tarehe 24 Februari 2017
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage,
Ameweka Jiwe la Msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Vigae cha Twyford (T) Chalinze.
Tarehe 17 Januari 2017
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Mh Charles Mwijage ameweka Jiwe la Msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kiwanda cha Sabuni
(Keds) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Kiwanda hicho ni cha pili kujengwa katika Bara la Afrika baada ya cha
kwanza kujengwa nchini Ghana.
Tarehe 04 Machi 2017
Tarehe March 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkr John Pombe Magufuli, ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kituo cha kupooza umeme
kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Wengine katika picha
ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo
Tarehe 22 Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya
Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akiwa na Waziri Maji
Mhandisi Gerson Lwenge, Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe pamoja na
viongozi wengine ameweka Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa
ujenzi wa mradi wa maji toka Ziwa Tanganyika
Mradi huo utagharimu Shilingi Bilioni
42 na utasambaza maji safi katika mji wa
kigoma unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Novemba 2017.
No comments:
Post a Comment