ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 5, 2017

UZINDULIWA wa Miradi 21+ KATI YA Novemba 5, 2015 na Novemba 5, 2017


UZINDULIWA wa Miradi 21+
 KATI YA
Novemba 5, 2015 na Novemba 5, 2017


 Matokeo chanyA+

Tarehe 06 Agosti, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe  kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga.
=============



Tarehe 29April 2017 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora,  mradi huo wa maji unafikia watu zaidi ya elfu 40 katika vijiji 32 mradi huu umedhaminiwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA.
=============

 
Tarehe 22 June, 2017 
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali alikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani.
==================



 
Tarehe 21Juni 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda cha nondo cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.
 ================


Tarehe 04Julai 2017 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine  akifungua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.

================

 

15 Aprili, 2017- Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ametekeleza Ahadi Yake Ya Kukabiliana Na Uhaba Wa Mabweni Kwa Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Ambapo amefungua Mabweni Mapya Ya Wanafunzi Yenye Uwezo Wa Kuchukua Wanafunzi 3,840.

Mhe. Rais Magufuli alitoa ahadi ya kujenga mabweni hayo 
tarehe 02 Juni, 2016 na ujenzi ukaanza tarehe 01 Julai, 2016 ambapo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamejenga majengo 20 yenye ghorofa 4 kila moja kwa gharama ya Shilingi Bilioni 10, na pia wamejenga uzio wa kuzunguka majengo hayo na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimenunua vitanda, makabati, meza, viti na magodoro kwa ajili ya wanafunzi wote 3,840.
===============

Tarehe 13Januari, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli amekata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo food product mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga.

================== 

Tarehe 13Januari, 2017- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli amekata utepe kwenye ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Compaany limited cha Mkoani Shinyanga. Kulia ni mmiliki wa Kiwanda hicho Fred Shoo.
 ==============

 
Tarehe 31 Oktoba, 2017 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefungua kiwanda cha Victoria molders and polybags kilichopo Igogo jijini Mwanza, kiwanda hicho pamoja na kiwanda dada cha Poly Bags vilivyopo katika eneo moja la Igogo vimeajiri watu 500 na vinazalisha bidhaa za plastiki ambazo ni Mabomba ya maji, matanki ya maji, ndoo, nyavu na mifuko ya kuhifadhia nafaka
============= 


Terehe 31 Oktoba, 2017 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefungua kiwanda cha madawa cha Prince Pharmaceuticals kilichopo Buhongwa nje kidogo jijini Mwanza.
 ===============
 

 
Tarehe 30 Oktoba 2017 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi kuashiria ufunguzi wa wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza.
===============


Tarehe 30 Oktoba 2017 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Nyakato Mjini Mwanza kilichojengwa na kampuni ya Kitanzania ya Motisan kwa gharama ya takribani Shilingi Bilioni 11 na Milioni 800.

Kiwanda hiki cha kisasa ambacho kimejengwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kina uwezo wa kuzalisha chupa 1,200 kwa dakika moja katika mitambo yake minne ya kuzalisha vinywaji baridi pamoja na chupa 100 za maji, kimezalisha ajira za watu 200 na kinaungana na kiwanda kingine cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Mboga Mkoani Pwani kusindika matunda ya wakulima na kuinua hali zao za maisha.
===============




  

Tarehe 06 Oktoba 2016 - Rais Dkt. Magufuli Amefungua Rasmi Kiwanda Cha Kusindika Matunda Cha Bakhressa Food Products Ltd. Mkuranga, Mkoa Wa Pwani  Kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda 13 vinavyomilikiwa na kampuni za Bakhresa vilivyopo Dar es Salaam na Pwani, kina uwezo wa kusindika tani 350 za matunda kwa siku, kimeajiri karibu wafanyakazi 1,000 na uwekezaji wake umegharimu takribani Shilingi Bilioni 261.

===============




 

Tarehe 22Juni 2017 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete

===============


 
Tarehe 22June 2017 -  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefungua kiwanda cha Matunda cha Sayona Fruits kilichopo Mboga Chalinze mkoani Pwani.
 =================

Tarehe 5 Machi 2017 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari makubwa ya kusafirishia Saruji kiwanda hapo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego  magari 580 ya kusafirisha saruji nchini yalimezinduliwa.
 =============



Tarehe 16 Februari 2017 - Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage amekata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanga cha utengenezaji wa viungo,Vegata Podravka Ltd,kilichojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 16.

==================


Tarehe 04 Machi  2017 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker wamekata utepe kuashiaria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Biashara cha Benki hiyo mkoani Mtwara.
===============


Tarehe 11 Septemba 2017 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage amekuwa

Mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Kiwanda cha kutengeneza mabati cha Kampuni ya ALAF Kanda ya Dodoma,

Kampuni ya ALAF (Tanzania) imefungua tawi lake jipya Mkoani Dodoma ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Sera ya Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma kwa wananchi baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.
Uwekezaji huu wa Dodoma ni wa thamani ya shilingi bilioni tatu ukiajiri watu 15 moja kwa moja na wengine zaidi ya 100 .
 ==================


 

Tarehe 25 Januari 2017 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amefungua Rasmi Wa Awamu Ya Kwanza Ya Miundombinu Na Utoaji Huduma Ya Mabasi Ya Mwendo Kasi.


Kukamilika kwa mradi wa mabasi ya mwendokasi wa awamu ya kwanza wenye kilometa 20.9 umetumia jumla ya shilingi bilioni 403.5 ambapo Tanzania imechangia bilioni 86.5 na Benki ya Dunia wametukopesha bilioni 317.
==============

Tarehe 28Septemba 2016 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam. 
============

 Inaendelea......

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments: