Mbunge wa jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye ameonyesha kukasilishwa na moja ya shabiki katika mtandao wake wa Twitter ambaye amemzihaki na kumwita mnafiki kutokana na ujumbe alioweka, Nape amedai watu wa namna hiyo ni zaidi wa wachawi.
Leo asubuhi Nape aliweka ujumbe kupitia mtandao wake unaosomeka "Usivunje mtungi kwa sababu ya panya aliyemo ndani ya mtungi, inamisha taratibu, fanya 'timing', utaua panya na mtungi utabaki salama"
Baada ya kuandika ujumbe huo ndipo moja ya mtu akaja na kumwambia kuwa kiongozi huyo amekua mnafiki baada ya kuvuliwa nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kudai kuwa kiongozi huyo amekuwa akiomkosoa boss wake, jambo ambalo Nape Nnauye wiki iliyopita alisema anachukizwa kuona watu wakichukua mambo yako na kuyahusisha na kumsema au kumkosoa Rais jambo ambalo si la kweli.
"Mkuu we mnafiki sana yote hayo umeanza baaada ya kuvuliwa uwaziri 'come on' kiongozi bora si yule anaonekana mkosoaji kwa boss wake" aliandika Majdy Wiliam
No comments:
Post a Comment