ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 5, 2017

WATANZANIA WASOGEZEWA MBELE FURSA ZA UWEKEZAJI NA MAENDELEO BANK

Wito umetolewa kwa wananchi kote nchini kuweza kujijengea utamaduni wa kuwekeza katika mfumo wa hisa na hasa katika hisa za Benki ya Maendeleo 
Wito huo kwa umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo, Ibrahim Mwangalaba jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kusogezwa mbele kwa zoezi lao la kuuza hisa za benki hiyo.Mwangalaba alisema njia kubwa ya kuwasaidia wananchi katika kujikwamua kimaisha ni kuchangamkiakia fursa zinazojitokeza ikiwemo ya kununua hisa za benki hiyo.Zoezi la uuzwaji wa hisa za benki hiyo ambalo lilianza Septemba 21, mwaka huu na lilikuwa limalizike leo sasa litandelea hadi Desemba 4, mwaka huu ili Watanzania wengi waweze kunufaika nalo.
Aliongeza kuwa lengo lao ni kuuza hisa zaidi ya mil.17 kwa Watanzania wapatao 170,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania..
Benki ya Maendeleo ni ya Watanzania wote, hivyo tumeona ni vema zoezi hilo lifanyike nchi nzima kwani awali tulikuwa tayari tumewafikia Watanzania kutoka mikoa 13 pekee na sasa tutatumia muda ulioongezwa kufika mikoa yote," alisema Mwangalaba.
Hisa moja inauzwa kuanzia sh.600 na kima cha chini cha kumiliki hisa ni 100.

No comments: