ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 29, 2017

HIZI NDIZO RASILIMALI NA MADENI YA ZITTO KABWE MWAKA 2017

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe leo amewasilisha Tamko lake la Rasimali na Madeni na Muswada wa Sheria kuwezesha Tamko la Mali na Madeni kuwa wazi kwa umma.

Zitto amefanya hivyo kwa mujibu wa ibara ya 132(4) na (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu cha 9 na 11 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka.

Zitto Kabwe Aanika Rasilimali na Madeni Yake

Mabadiliko mengine ni, kuongezeka kwa rasilimali ambazo ni hisa 60,000 za Kampuni ya Vodacom na kupimwa kwa ardhi eneo la Mangamba Manispaa ya Mtwara Mikindani 42 surveyed and tittled plots).

Taarifa ya zito ya mwaka 2017, inatofauti ndio na taarifa ya mwaka 2016. Utofauti huo unaonekana katika, kuongezeka kwa deni jipya kutoka Benki ya Azania tshs 104 milioni na deni la mtu Binafsi la $2300, kupungua kwa madeni ya CRDB kutoka tshs 214 milioni kufikia tshs 143 milioni na NSSF tshs 142 milioni kutoka 191 milioni baada ya kuyalipa kwa mwaka mzima uliopita.

ZITTO KABWE ATOA TAMKO KUHUSU KUWEKWA WAZI RASILIMALI NA MADENI YA VIONGOZI, AGUSIA MSHAHARA WA JPM
GPL

No comments: