Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna akizungumza na waandishi wa habari
Na Mwandishi Wetu, Pwani
MTU mmoja nayesadikiwa kuwa ni jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kubainika kumjeruhi dereva wa Bajaji aliyefahamika kwa jina la Looqman Salehe mkaazi wa Mwanalugali Wilayani Kibaha Mkoani Pwani katika tukio lililotokea majira ya saa moja usiku maeneo ya Machinjio ya zamani huku majambazi hayo wakitoweka na Bajaji hiyo.
Imeelezwa kuwa watu hao walimfunga kamba dereva huyo wa Bajaji yenye usajili namba MC 415BSH na kwenda kumtupa eneo la Pangani alikoolewa na wasamaria wema waliokuwa wakipita katika eneo hilo.
Baada ya taarifa kufikishwa katika Jeshi la Polisi Mkoani Pwani walichukua hatua za haraka za kuweka mitego katika maeneo mbalimbali na kuwashirikisha wananchi na kuendesha msako mkali mtaa kwa mtaa,hatimaye wezi hao waliingia katika mtego, yamesemwa hayo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna alipozungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika kwenye kituo cha Polisi Mapinga Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Kamanda Shanna amewataka wahalifu waliokimbia kujisalimisha mara moja kwani Jeshi la Polisi limeshapata taarifa za uhakika kutokana na kubaini maeneo wanayoishi.
No comments:
Post a Comment