Mwanamziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Money Mondays itakayofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo "Mohombi" akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa albamu ya kwanza ya Vanessa Mdee inayokwenda kwa jina la Money Mondays pamoja na ushirikishwaji wake kwenye baazi ya nyimbo za kwenye albamu hiyo.
MWANAMUZIKI maarufu nchini katika muziki wa Bongo Fleva Vanessa Mdee hatimaye amezindua albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Money Mondays.
Albamu hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam leo na miongoni mwa wanamuziki walishuhudia sherehe za uzinduzi wa albamu hiyo ni msanii wa kimataifa Mohombi.
Kwa kukumbusha Mohombi siku za karibuni ameshinda tuzo ya kimataifa ya Grammy mwenye uraia wa Sweden na Congo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Vanessa amesema katikka albamu hiyo wameshirikishwa nyota kadhaa wa muziki akiwamo Joh Makini, Caspper Nyovest wa Afrika Kusini, Konshens wa Jamaica na nyota wa tuzo ya kimataifa ya Grammy Mohombi.
Amesema albamu hiyo ni ya kwanza kwake na tayari imeshapata umaarufu mkubwa kutoka kwa mashabiki na kutabiriwa kuwa moja ya albamu kubwa kwa mwaka 2018.
Uzinduzi wa albamu hiyo umesimamiwa na kuratibiwa na Mikito App ambao wameonesha sapoti kubwa.”Sambamba na wadhamini wengine kama Mdee Music ,GSM Travel and Tours,Hyatt Kilimanjaro hotel na Henney”.
Pia ametumia uzinduzi wa albamu yake mpya yenye nyimbo kama Kwangu njo ailiyomashirikisha Mohombi amethibitisha ubora wa muziki wake na kipaji chake katika kuimba kwa hisia.
Vanessa Mdee kwa siku za karibuni amekuwa moja ya wasanii wakike wenye uwezo mkubwa kimuziki na amefanikiwa kutikisa katika anga la muziki wa kimataifa kupitia nyimbo zake kadhaa.
Wakati akiwa leo ndio ameizindua albamu hiyo tayari imeshaana kutajwa kuwa moja ya albamu bora ambazo zilikuwa zikitarajiwa na mashabiki.
Katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda vema , anatarajia kufanya ‘Party’ maalum leo katika hoteli ya Hyatt Dar es Salaam kwa waalikwa maalumu kwa ajili ya kuisikiliza albamu hiyo na mgeni rasmi atakuwa Mohombi.
No comments:
Post a Comment