Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dk. Adelardus Kilangi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu (AfCHPR)Jaji Sylvain Ore walipokuta Jijini Arusha. Katika mazungumzo yao, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliahidi kushirikiana wa Mahakama hiyo ambapo kwa upande wake Rais wa AfCHPR alisema mahakama hiyo imekuwa ikipata ushirikiano mzuri kutoka kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa Mawakili wa Serikali ambao wamekuwa wakiiwakilisha serikali katika mashauri mbalimbali.. Mwingine katika picha ni Katibu wa Mwanasheria Mkuu, Wakili wa Serikalil Mkuu Ephery Sedekea.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dk, Adelardus Kilangi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ( EACJ), Mhe Jaji Dk. Emmanuel Ugirashebuja na katika mazungumzo yao Rais wa EACJ alimweleza Mwanasheria Mkuu kwamba mahakama hiyo imekuwa ikizitegemea Ofisi za Wanasheria Wakuu ikiwamo ya Tanzania katika utekelezaji wa Majukumu yake.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akijadiliana jambo na Majaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika ya Mashariki (EACJ) wakati alipoitembelea mahakama hiyo leo Ijumaa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiangalia namna mfumo wa habari na mawasiliano wa mahakama hiyo unavyofanya kazi wakati alipoitembelea Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki leo Arusha
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dk.Adelardus Kilangi, amesema, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, itaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu ( AfCHPR) pamoja na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ( EACJ).
Ametoa uhakikisho huo kwa nyakati tofauti wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Marais wa Mahakama hizo Jijini Arusha, akiwa katika ziara ya kujitambulisha.
" Napenda niwahakikishie kwamba, Serikali na Ofisi yangu tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi nanyi ili kwa pamoja tutekeleze majukumu yaliyombele yetu kwa ufanisi na katika ukamilifu wake". Akasisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa upande wake Rais wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki Mhe. Jaji Dk.Emmanuel Ugirashabuja, amemueleza Mwanasheriak Mkuu wa Serikali kwamba, Mahakama hiyo inazitigemea Ofisi za Wanasheria Wakuu wa Serikali ikiwamo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Tanzania katika utekelezaji wa majukumu yake na kwamba, ushirikiano baina ya pande hizo mbili ni jambo la muhimu sana.
Naye Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu, Mhe.Jaji Sylvain Ole amebainisha kuwa Mahakama hiyo imekuwa ikipata ushirikiano mzuri kutoka Tanzania ikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
" Tumekuwa tukipata ushirikiano mzuri kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo Mawakili wa Serikali wamekuwa wakiiwakilisha vema Serikali katika Mashauri mbalimbali". Amesisitiza Jaji Sylvan Ole.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali moja ya majukumu yake ya msingi ni kuiwakilisha Serikali katika mashauri mbalimbali yanayofunguliwa dhidi ya serikali katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki na Mahakama ya Afrika ya Haki za Watu na Binadamu.
Katika ziara yake hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali pia alipata fursa ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa mahakama pamoja na mfumo wa habari na mawasiliano wa mahakama hiyo unavyofanya kazi.
No comments:
Post a Comment