ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 20, 2018

16 wanashikiliwa na polisi kwa mauaji na wizi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikiliwa watu 16 kwa uchunguzi baada ya kubainika kujihusisha na matukio mawili tofauti likiwamo la kumsababishia kifo cha Charles Msangwa (65) aliyeuawa kwa kupigwa fimbo wakati akiamua mgogoro wa kifamilia.
Akizungumza leo Jumanne Machi 20, 2018 Kamanda wa Polisi Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea Machi 17, 2018 saa 11 jioni katika Zahanati ya Katoro iliyopo wilayani huo.

Amesema marehemu akiwa nyumbani kwake aliitwa na mtoto wa nyumba jirani akiomba msaada wa kuamua ugomvi kati ya Mashaka Sizya na baba yake Sizya Lusalya.
Amesema wakati Charles akiamua ugomvi huo, alipigwa fimbo kifuani na kukimbizwa katika Kituo cha Afya Katoro lakini alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda amesema miongoni mwa watuhumiwa hao, sita wameshapandishwa mahakamani huku wengine tisa wakiendelea kuhojiwa na uchunguzi utakapokamilika watapandishwa mahakamani.

Chanzo: Mwananchi

No comments: