ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 21, 2018

Kamati ya kitaifa ya UN na Serikali yakutana kupanga kazi za mradi wa Koica

 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kuhaisa (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo (kulia) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou  kwa pamoja wakipitia ratiba ya mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Jennifer Kotta akitoa neno la ukaribisho na kutambulisha meza kuu wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou, mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo, Kaimu Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa KOICA nchini, Joonsung Park.
 Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkazi wa KOICA nchini, Joonsung Park ambao ndio wafadhili wa mradi huo akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kuhaisa akizungumza kwa niaba ya Anne Theresa  Ndog-Jatta wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou akitoa salamu za UN WOMEN katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo kwa mwaka 2018 unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na KOICA uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kubaisa (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo (katikati) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Hodan Addou (kushoto).
 Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Jennifer Kotta akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Afisa Programu anayeshughulikia masuala ya Afya ya Uzazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Fatina Kiluvia akishiriki katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2018 unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na KOICA ambao umefanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
 Afisa Programu anayeshughulikia Utawala wa Kidemokrasia wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women), Rachael Boma akichangia jambo wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkazi wa KOICA nchini, Joonsung Park akiuliza swali baada ya wasilisho la Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) nchini, Jennifer Kotta wakati wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kuhaisa akishiriki mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi  wa Mafunzo na Maendeleo ya Utalaamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Venerose Mtenga akijibu swali katika mkutano wa kujadili mwelekeo wa mradi unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na KOICA ambao umefanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
 Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Salim Sururu akichangia wakati wa mkutano wa kujadili mwelekeo wa mradi kwa mwaka 2018 unaohusu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu unaofadhiliwa na KOICA uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya UN na Serikali ya mradi wa unaofadhiliwa na KOICA wa kuendeleza wasichana na wanawake vijana kielimu uliofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

KAMATI ya kitaifa inayoendesha mradi wa pamoja kati ya mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa (UNESCO, UN Women na UNFPA) na serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na wizara nyingine ambazo zinahusika na maswala ya Elimu hususani TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maedeleo ya Jamii, Jinsia, Watu Wazima na Watoto na Wizara ya Sheria na Katiba pamoja na mfadhili wa mradi KOICA imekutana kwa mara yake ya kwanza kujadili mwelekeo wa mradi unawo husu kumwendeleza msichana na mwanamke kijana kupitia elimu.

Mkutano huo uliokuwa chini ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo uliangalia na kubadilishana mawazo ya hatua zilizofikiwa katika mradi huo ulioanza mwaka 2016 na kutekelezwa katika wilaya nne nchini Tanzania (Kasulu, Ngorongoro, Sengerema na Mkoani, Pemba) kwenye kata 22 na kupitia mpango wa mwaka 2018.

Akizungumza kabla ya kusimamia mazungumzo, Dk Akwilapo aliwashukuru wafadhili na pia wadau wengine waliojipanga kufanikisha mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wanawake nchini Tanzania na uchumi kwa ujumla.

“Mradi huu ni muhimu sana kwetu, kwa kuwa unachangia juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) na wizara nyingine zinazofanyakazi kwa pamoja bila kuchoka kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu zikiwemo Wizara za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu na Wizara ya Katiba na Sheria MoCLA” alisema.

Alisema wizara hizo zimekuwa zikifanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba taifa linatoa elimu yenye ubora na kusaidia wale waliopo pembezoni wanapata elimu hasa wasichana na wanawake vijana ambao hawako shuleni kwa sababu mbalimbali.

Aliongeza kwamba uwepo wa kamati hiyo na mikutano yake ni matokeo ya makubaliano yaliyoanzisha programu hiyo ya kusaidia wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, ambapo pia kuna kamati ya ufundi inayotangulia mkutano wa kamati ya kitaifa.

Kamati ya ufundi ilikutana Februari Mosi mwaka huu katika ofisi za Unesco, Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, nia ya mkutano wa kamati ni kuhakikisha kwamba mradi huo kwa kushirikiana na wizara husika unatekelezwa katika ubora unaotakiwa.

Aidha aliwataka wadau waliohudhuria mkutano huo wakiwemo wajumbe kutoka serikali ya mapinduzi Zanzibar kuhakikisha kwamba wanaangalia utekelezaji wa mradi huo kwa makini kwa manufaa ya umma wa Tanzania.

Aliwataka wadau waelewe kama mradi huo ni wakwao ili kupatikane mafanikio yanayotarajiwa.

Aidha alisema kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuboresha sera za elimu kwa lengo la kuifanya elimu inayotolewa kuwa bora zaidi.

Alisema serikali inaelewa vikwazo vinavyowaondoa wasichana shuleni ikiwamo mihemko ya ujana na utamaduni wa baadhi ya maeneo na kusema juhudi lazima zifanyike kuhakikisha kwamba hali hiyo haiendelei kuwapo na wale walioshindwa wanaendelezwa kwa namna nyingine.

Alisema ipo haja ya kuwezesha mazingira rafiki ya usomaji kwa watoto wa kike kwa kuweka tabia chanya miongoni mwa walimu na wazazi kuhusiana na malezi ya watoto wa kike.

Alisema serikali inataka kupunguza mdondoko wa wananfunzi na pia kuwasaidia waliopata bahati mbaya hiyo na kujikuta nje ya mfumo rasmi wa elimu.

Pia iliongeza kuwa serikali inatambua juhudi zinazofanywa na wadau wa maendeleo kama UNESCO, UN Women, UNFPA na KOICA, na kusema itaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa lengo la kuboresha hali ya wasichana na wanawake vijana.

Naye mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki, Viola Kubaisa alisema kwamba mkutano huo wa mashauriano kwa mradi huo unaoendeshwa Ngorongoro, Mkoani Pemba, Kasulu na Sengerema ni muhimu kwa kuwa unapanga mpango kazi na kuangalia namna bora ya utekelezaji wa mradi huo.

Viola akizungumza kwa niaba ya Anne Theresa  Ndog-Jatta, alisema kwamba baada ya kukamilika kwa kampeni dhidi ya ukeketaji katika wilaya ya Ngorongoro mwaka jana katika kutekeleza lengo la maendeleo endelevu ya dunia namba 4.7; na utengenezaji wa kitini cha kufunzia walio nje ya mfumo rasmi wa masomo (kazi inayofanywa na UNFPA na Ofisi ya Waziri Mkuu) kunasaidia kuwapo kwa msingi thabiti wa kusaidia wasichana na wanawake vijana kufikia ndoto zao.

Pia mambo mengine yanayokwenda sanjari na mradi huo ni mahusiano kati ya UN Women na Wizara ya Katiba na Sheria ambapo masuala ya sheria zinazokandamiza wanawake yanashughulikiwa.

Naye Kaimu Mkuu wa Ofisi za Unesco nchini, Faith Shayo alisema kwa mujibu wa utekelezaji wa mradi huo wa kusaidia wasichana na wanawake vijana, kamati hiyo ni ngazi ya juu ya maamuzi ya utekelezaji wa mradi huo na kazi yake kubwa ni kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na malengo yake yanafanikiwa.

No comments: