ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 19, 2018

AWAMU YA TANO YA RAIS DKT. MAGUFULI YAWATUA NDOO WANANACHI WA GAIRO

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kulia) na wageni wake kutoka Sweden wakishiriki msaragambo na wanawake wa Kata ya Chakwale kuchimba mtaro wa kutandaza mabomba ya Maji.
Mhandisi Magumbo (wa kwanza kushoto) anayekuwa akisimamia mradi huo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Mchembe (katikati) na wafadhili kutoka nchini Sweden mara baada ya kufika kukagua.
Mhandisi wa Wilaya ya Gairo Heke Bulugu akitoa ufafanuzi kwenye baadhi ya mambo.
Wadau mbalimbali wakiwemo Madiwani na Watendaji wa Kata. Neema ya Mradi wa Maji safi na Salama Gairo chini ya uongozi makini wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli unaendelea kwa kasi ya ajabu.

Akitembelea mradi Maji Safi na Salama uliopo Gairo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Mchembe akiwa ameongozana na Mhandisi wa Maji Wilaya Eng. Heke Bulugu, Madiwani wa Chakwale na Madege pamoja na Watendaji wao, na Mhandisi wa Lions Pure Water Eng. Magumbo pamoja na wafadhili wa kutoka nchini Sweden; Mhe. Mchembe ameeleza kuwa Mradi huo unahudumia kata 2 za Madege na Chakwale na vijiji 6 vya Madege, Ng'olong'o , Sanganjelu, Chakwale, Kilimani na Kimashale.

Aliongeza kuwa utanufaisha jumla ya wananchi 10,358 kwa gharama ya shs 348,000,000/- kwa mchanganuo ufuatao Lions Pure Water shs 278,000,000/- Halmashauri kupitia Serikali kuu shs 48,000,000/- na Nguvu za wananchi 22,000,000/-

Mhe. Mchembe ameisifia serikali ya Rais Dkt. Magufuli ya hapa Kazi tu! kwa kuweza kuwajali wanyonge kwa kuwatua ndoo kichwani akinamama.

No comments: