ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 19, 2018

Taesa yatoa ufafanuzi jinsi ya kujisajili ajira 10,000 bomba la mafuta

Kufuatia Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi “East Africa Crude Oil Pipeline (EACOP)” kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, Taesa imetoa ufafanuzi namna ya kujisajili na ajira hiyo ili kuweza kutambulika.
Mradi huo ambao ujenzi wake unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 24 hadi 36, unategemewa kuzalisha fursa za ajira takribani 10,000 wakati wa ujenzi na ajira zaidi ya 1,000 wakati wa uendeshaji wake.

Hivyo Watanzania wote wenye taaluma na ujuzi katika Sekta ya Mafuta na Gesi  wanatakiwa kujisajili TaESA kwa kuingiza taarifa zao lengo likiwa kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya Watanzania walio na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi huo.

Zoezi la usajili limekwishaanza na linatarajiwa kukamilika tarehe 30/03/2018, na usajili unafanyika kwa kujaza fomu maalumu inayopatikana katika tovuti ya www.taesa.go.tz, au kwa kufika kwenye ofisi zao za kanda zilizoko Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.


Fomu zilizojazwa zinaweza kuwasilishwa kwenye ofisi zao za kanda au kwa barua pepe: eacop@taesa.go.tz. Kwa maelezo zaidi wasaliana nao kupitia namba zifuatazo: 0736 551 055; 0739 221 022; 0735 221 022; 0735 551 055 na 0282 541 840/1.

Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa kutekelezwa nchini, unaotegemea kugharimu Dola za kimarekani 3.5 sawa na bilioni 8 za kitanzania

Bomba hilo litakuwa na urefu wa wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba hilo utafanyika nchini Tanzania. 

Jumla ya wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.

No comments: