ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 12, 2018

CHAMA TAWALA CHINA CHAIDHINISHA ‘RAIS WA MAISHA’

Rais wa china Xi Jinping.

Chama tawala cha National People’s Congress nchini China, kimeidhinisha marekebisho ya kipengee cha katiba, ya kufutilia mbali uongozi wa mihula miwili kwa Rais wa nchi hiyo.
Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023 na kuendelea kuongoza kwa kipindi kisichojulikana.

Waandishi habari walinyimwa idhini ya kuingia Bungeni, kushuhudia zoezi hilo la kupiga kura likifanyika.

No comments: