ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 15, 2018

NAOMBA KURA YAKO NAFASI YA MKURUGENZI WA BODI JUMUIYA YA WATANZANIA DMV


NDUGU ZANGU WANA DMV Mimi mwanaJumuiya mwenzenu Zena Janu, nachukua nafasi hii kuwaomba kura zenu za ndio ili niweze kutumikia katika Bodi ya Wakurugenzi kwenye Jumuia yetu. 



Mkinipa ridhaa hiyo, nitashirikiana na viongozi wote watakaochaguliwa kusimamia uongozi utakaochaguliwa ili kuhakikisha mahitaji na matakwa ya wana DMV yanatekelezwa. - 



Pia nitahakikisha kuwa maamuzi yetu yanafanyiwa kazi kulingana na Katiba yetu katika kulinda haki za kila mwanajumuiya. Kwa pamoja tuijenge *DMV yenye Umoja, Upendo, Heshima na Mshikamano.* Kwani sisi ni wamoja. Asanteni

No comments: