Habari wana DMV, Jina langu naitwa Lysa Bantu. Nimeamua kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Watanzania tunaoishi DMV. Kutokana na uzoefu pamoja na taaluma yangu, nimeomba kugombea nafasi ya Mweka Hazina. Naomba kura yako pamoja na, ushirikiano wako ili kuniwezesha kufanikisha dhamira yangu. Nina amini ya kwamba uzoefu wangu, utaalamu na maarifa niliyoyapata kwa kufanyakazi katika benki iliyo katika kundi la benki 10 bora hapa Marekani imenipa uwezo mkubwa wa kuhudumia Jumuiya yetu ya hapa DMV.
Utakapo nipigia kura siku ya tarehe 24 machi 2018. Utakuwa umeunga mkono azimio la kuleta DMV mpya yenye Upendo, Kuheshimiana,Kusaidiana na kushiriakiana.
Naomba uwaombe ndugu na marafiki wanipe kura zao ili niweze kuwatumikia.
Wakumbushe kujiandikisha kupiga kura.
Natanguliza shukrani.
No comments:
Post a Comment