Shirikala Kimataifa la La Francophonioe (OIF) ambalo linajumuisha nchi 84 ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa limesema kwamba ni muhimu kwa
Watanzania kujifunza lugha ya Kifaransa kwa sababu kuna fursa nyingi
wanaweza kuzipata kwa kuzungumza lugha hiyo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25, Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier amesema katika nchi hizo kuna nafasi za kazi nyingi
ambazo kama Watanzania watajifunza Kifaransa wanaweza kuzipata.
Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier akizungumza kuhusu Wiki ya Francophonioe ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25.
"Hapa Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili
linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa
wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu
waitumie."
"Tanzania inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza Kifaransa," alisema Clavier.
Aidha, Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania
kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF
ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française,
Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo
Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment