ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 17, 2018

TCRA:EPUKENI KUWEKA TAARIFA NYINGI ZINAZOWAHUSU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu

Na.Vero Ignatus. Arusha
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Katika kuadhimisha siku ya walaji duniani inayo adhimishwa kila mwaka machi 15 kila mwaka imetoa mafunzo kwa waalimu wanafunzi zaidi ya 300 katika chuo cha ualimu Monduli mkoani Arusha.

Akizungumzia Madhumuni ya kutoa elimu hiyo Kaimu meneja wa Mamlaka ya mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu amesema ni katika jitihadha zilezile za serikali za kuhakikisha kwamba inamlinda mlaji kwa kumpa elimu juu ya haki na wajibu wawatumiaji wa huduma za mawasiliano kwaajili ya kuleta maendeleo.

Katika kuadhimisha siku ya walaji wameitumia kutoa elimu juu ya haki, na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano kama sehemu ya walaji,tahadhari za kuchukua katika mawasiliano hususani mitandao.

Msungu amesema kwamba walaji,ni kundi kubwa la kiuchumi ambalo huwa linaadhirika na kuathiri maamuzi ya kiuchumi yanayofanywa na mataifa na makampuni ya kibiashara.

"Sisi kundi hili la walaji ni kundi lile ambalo maoni yetu huwa usual a to kusikilizwa kwa makini katika maamuzi ambayo yanafanywa ya kiuchumi" alisema.


Kwa upande wake Mhandisi Mwandamizi wa Masafa (TCRA) Jan Kaaya ametoa tahadhari kwa jamii kutokuweka taatifa nyingi zinazowahusu kwenye mitandao kwani siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la uhalifu ambalo wanatumia mitandao kufuatilia taarifa za watu.

Jan amesema ni muhimu kuhakikisha unapoweka taarifa ako katika mitandao hii ya kijamii,usiweke taarifa zako nyingi zinazomiwezesha mtu kuzitumia hizohizo katika kukudhuru wewe mwenyewe.

Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini Julius Filex Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini Julius Filex amezungumzia suala la uninuzi wa simu na kisema kuna sheria ya Mawasiliano ya kieletroniki na posta ya mwaka 2010/ambayo inamtaka mnunuzi wa simu kuhakikisha baadhi ya vitu kabla hajakabidhiwa simu.

Ahakikishe amepewa risiti,garantiibya mwaka mzima,auziwe simu ikiwa kwenue box lake,pia aangalie simu yake ni bandia ama la kwa kutumia *#06
Mhandisi Mwandamizi wa Masafa (TCRA) Jan Kaay akizungumza na waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kaimu mkuu wa chuo cha Ualimu Monduli Jesca Moiro akizungumza katika mafunzo hayo kama mwenyeji wa wanafunzi waalimu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini (wa kwanza kulia) Julius Filex akizungumza na waalimu wanafunzi katika chuo cha ualimu Monduli ,(kushoto )Afisa kutoka (TCRA) Osward Octavian akionyesha vitabu ambavyo ni muongozo kwa watumiaji wa mawasiliano.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya washiriki ya mafunzo hayo yaliyoandaiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA) nakufanyika katika chuo cha Ualimu Monduli mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.

No comments: