ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 12, 2018

Teknolojia ya kinuklia inaokoa mahindi

Kilimo katika Tanzania ni muhimu sana kwa uchumi na unachangia asilimia 30 hivi katika pato la taifa na zaidi ya asilimia 50 za ajira. Sekta nzima inaendelea sana. Kutokana na kielezo cha uzalishaji wa mazao cha Benki ya Dunia, uzalishaji wa mazao wa Tanzania umeongezeka kwa asilimia 44 toka mwaka 2008 mpaka mwaka 2013 na kiwango cha ukuaji wa wastani katika Afrika Kusini ya Sahara ni asilimia 18. 
Miongoni mwa mazao mahindi inachukua mahali maalum katika usalama wa chakula. Tanzania ipo miongoni mwa nchi 25 zinazoongoza ukulima wa mahindi. Mahindi ni zao lililo muhimu zaidi katika Tanzania na linachukua zaidi ya asilimia 40 za ardhi inayolimwa nchini. Uzalishaji wa mahindi ni zaidi ya asilimia 70 za nafaka inayozalishwa nchini. 
Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 85 na 90 za wenyeji wa Tanzania, ambao ni watu milioni 50, wanakula asilimia 90 za mahindi. Inayobaki inauzwa nje katika nchi za jirani. Asilimia 80 za mahindi zinalimwa na wakulima wadogo kwaajili ya chakula na uuzaji. 
Ili kuhakikisha mazao mazuri na usalama wa chakula wa siku ijayo lazima kuhifadhi mabegu na mimea ya mahindi. 
Hivi karibuni mamia ya hekta za mahindi yalivamiliwa na kiwavijeshi na wadudu wa majani ya mahindi ambao ni hatari kubwa kwa mazao. Kutokana na Innocent Keya ambaye ni afisa wa ukulima wa mkoa wa Mwanza, mwishoni mwa mwaka 2017 zaidi ya hekta 7500 ziliangamizwa na wadudu hao. 
Siku hizi mikoa Kaskazini ya Tanzania inatishwa na uvamizi wa wadudu. Ili kuzuia athari mbaya za wadudu hao watu wanatumia mibinu ya kawaida na isiyo ya kawaida. Wakulima wanaweza kutumia viuavisumbufu nyingi sana lakini vinaathiri mazingira sana na baada ya muda flani wadudu hawajali viuavisumbufu zaidi. 
Vinginevyo inawezekana kutumia teknolojia ya kinuklia ili kukabili wadudu bila ya kuharibu ardhi na mazingira.
Shirika la Nishati ya Kinuklia la Kimataifa (IAEA) linatumia sayansi ya kinuklia kuendeleza mbinu mpya wa kupiga wadudu bila ya kuharibu mazingira. IAEA pamoja na Shirika la Kimataifa la Chakula na Ukulima (FAO) yanadhamini miradi na uchunguzi katika udhibiti wa wadudu kwa kutumia mnururisho wa ioni. Mashirika hayo yanasisitiza umuhimu wa Teknolojia ya Wadudu Gumba (SIT) ili kushindana na wadudu kama kiwavijeshi.
Mnururisho unatumika kudhibiti ukubwa wa madudu kwa kutumia SIT. Teknolojia inahusika na wadudu wengi sana wanaotasishwa na mnururisho wa aina ya gamma na x-ray na baadaye wadudu wanarudishwa katika mazingira yao. Teknolojia ya SIT haiharibu mazingira na imehakikishwa kuwa SIT inafaulu kupiga wadudu hata katika mahali ambapo utumiaji wa viuavisumbufu havikufaulu. 

No comments: