Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuwapelekea mafundi wa ujenzi kwa ajili ya ukamilishaji wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 katika mji wa Malinyi, ( kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda akichanganya saruji na mchanga kwa ajili ya ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuchanganya mchanga na saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 mjini Malinyi na ( kushoto kwake ) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda , na ( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa wilaya hiyo Majura Kasika.
Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji , Jumaa Aweso, akimsiliza Mzee Said Mazinge wa Kata ya Kibati, wilaya ya Mvomero , mkoa wa Morogoro kuhusu changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama alipofanya ziara wilayani Mvomero.
Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa mji wa Mlimba , wilaya ya Kilombero juu ya azma ya serikali ya awamu ya tano ya namna ya kutatua changamoto za ukosefu wa maji maeneo ya vijijini na mijini.
Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso akipambu maji katika moja ya kisima kirefu mara baada ya kukizundia katika kijiji cha Chikuti, wilaya ya Ulanga kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa kijiji hicho .
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini , Abdulaziz Abood ( kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso kwenye Ofisi ya Dc Morogoro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ( kushoto) akitoa shukrani zake kwa mapokezi katika Ofisi ya CCM wilaya ya Morogoro Mjini. ( mwenye furana ya pundamilia ) ni Mbunge wa Jimbo la Moro Mjini, Abdulaziz Abood.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ( mwenye kofia ) akiangalia sehemu ya uendeshaji wa mitambo ya kuchuja maji eneo la chanzo cha maji Mambogo, Manispaa ya Morogoro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwahutubia wananchi katika kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro kuhusu mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya kumtua ndoo kichwani mwanamke kwa kusogeza huduma bora za maji safi na salama.
Sehamu ya umati wa wananchi wa Kata ya Lukobe, Kihonda, na Mkundi katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni miongoni mwa kata tano kati ya 29 zinazokabiliwa na uhaba mkubwa wa maji wakimsililiza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, ( hayupo pichani) wakati akielezea mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya kumtua ndoo kichwani mwanamke kwa kusogeza huduma bora za maji safi na salama.( Picha zote na John Nditi).
Na John Nditi, Morogoro
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imesema ili kuleta ufanisi mkubwa katika usimamizi wa miradi ya maji safi na salama vijijini, ipo haja ya kuwa na chombo cha kusimamia huduma za maji vijijini utakaosimamiwa na wizara kwa lengo la kuleta uwajibikaji wa karibu kwa watumishi wanaosimamia sekta ya maji nchini.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Jumaa Aweso alisema hayo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali kikiwemo cha Dumila juu katika Kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Kabla ya kuzungumza na wananchi alipata fursa ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji Dumila ambao ulianza kujengwa tangu Januari 24, 2014 na kukamilishwa Desemba 15, 2017 kwa gharama ya Sh milioni 800.5.
Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya wiki moja mkoani Morogoro iliyomfikisha katika halmashauri za wilaya sita kati ya tisa ambazo ni Malinyi, Ulanga, Kilombero, Mvomero, Manispaa ya Morogoro na Kilosa .
Alisema kuwa, miradi mingi ya maji safi na salama inayotekelezwa vijijini imekosa usimamizi wa karibu, ufanisi na mingi imejengwa chini ya viwango na baadhi katika maeneo ambayo vyanzo vyake vya maji si vya kuaminika.
Alisema kuwa , endapo miradi mingi ya maji saji na salama iliyoanzishwa na kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini ingetoa matokeo mazuri ya maji kam ilivyokusudiwa na serikali , wananchi wangeondokana na changamoto za uhaba na ukosefu wa maji safi na salama.
Hata hivyo alisema , ili kuleta ufanisi na usimamizi wa karibu katika miradi ya maji safi na salama kwa wananchi vijijini katika kufikia azma ya serikali ya kuwatua ndoo kichwani mwanamke kwa asilimia 85 wakazi wa vijijini na asilimia 95 wa mjini kuna haja ya kuwa na chombo kitakachosimamia maendeleo ya Maji Vijijini.
Pmoja na hayo alisema kuwa, baadhi ya wataalamu washauri wa miradi ya maji , wakandarasi na wahandisi wa maji ngazi za mikoa na wilaya wanachangia kuhujumu serikali kutokana na kupeana kazi kwa njia ya ujanja ujanja na kuiibia serikali fedha kwa kushindwa kukamilisha miradi ya maji kwa wakati ..
Hivyo alisema , wizara itachukua jukumu la kuorodhesha makampuni ya washauri wa miradi ya maji na ukandarasi wa ujenzi yatakayobainika kuihujumu serikali kwa kutoa ushauri mbovu ama kujenga miradi chini ya kiwango ili Bodi ya Wakandarasi iweze kuwachukulia hatua za kuwafutia usajili wao.
“ Wizara itaanza hatua za kisheria dhidi ya wakandarasi wa miradi ya maji watakaobainika wanaihujumu serikali kutokana na kukosa sifa ya kuwa wakandarasi na kujenga miradi chini ya kiwango na kusababisha ucheleweshaji wa jitihada za kuwafikishia wananchi huduma ya maji karibu vijijini na mijini” alisema Aweso.
“ Miradi ya Maji safi na salama na ile ya Umwagiliaji inakuwa ikitumia fedha nyingi za serikali, lakini mingi haileti matokeo yanayokusudiwa kwa wananchi nahujumiwa na kusababisha wananchi wanjenga chuki na serikali yao” alisema Aweso.
Alisema , katika ziara yake katika mkoa amebaini kuna hali ya kuindana na kuwaomba madiwani wa halamshauri za wilaya hizo kuchukua hatua kwa mtaalamu yoyote anayewahukumu kwa kuwa Baraza la Madiwani ina nguvu ya kuchukua hatua dhidi ya wataalamu wa sekta mbalimbali kwenye halmashauri.
Naye Kaimu Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Morogoro anayeshughulikia maji ,Mhandisi Beatrice Kasimbazi alisema , Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imelipa kiasi cha Sh bilioni 4.2 zikiwa ni fedha za madeni ya wakandarasi , usimamizi , uandaaji na uendeshaji wa vyombo vya watumia maji (COWSOs) pamoja na Usafi wa Mazingira kwa mkoa wa Morogoro.
Alisema kuwa , juhudi za serikali ya awamu ya tano za kulipa madeni zimewezesha wakandarasi wote walikuwa wamesimama kutoka na ukosefu wa fedha , kurudi katika maeneo ya miradi ambapo kwa sasa ukamilishaji unaendelea kwa kasi kubwa.
Mhandisi Kasimbazi alisema , katika kipindi cha mwaka wa 2017/2018 kiasi cha fedha kilichopolekewa kwenye halmashauri za mkoa wa Morogoro ni Sh 4,220,974,569 : 24.
Kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya kulipia gharama za wataalamu washauri, kuchimba visima vya maji , umasishaji kuhusu usafi wa mazingira , usimamizi na ufuatiliaji, uendeshaji wa ofisi na ujenzi wa miradi ya maji katika baadhi ya vijiji 10.
Hata hivyo alisema fedha zilizotengwa na serikali kuu katika bajeti kwa ajili ya programu ya maji kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ilikuwa ni sh 11,605,687,000 kwa ajili ya halmashauri za wilaya tisa za mkoa huo.
Alisema ,licha ya mipango mizuri ya Serikali ,mkoa unakabiliana na changamoto mbalimbali katika utoaji wa huduma za maji , ikiwemo upungufu wa wahandisi na mafunzi sanifu kwa ajli ya usanifu ,usimamizi na uendeshaji wa miradi.
Kaimu Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Morogoro anayeshughulikia maji alisema , mkoa una wahandisi 13 na mahitaji halisi ni wahandisi 34 na upungufu ni wahandisi 21 , mafunzi sanifu waliopo ni 21 na mahitaji 70 hivyo upungufu ni 49.
Mhandisi Kasimbazi alitaja changamoto nyingine uwezo mdogo wa wakandarasi katika kutekeleza miradi ya maji kwa wakati na kufanya huduma ichelewe kutolewa kwa wananchi.
Pia alitaja uchafuzi wa vyanmzo vya maji unaofanywa na wakulima na wafugaji kwenye vyanzo vya maji ikiwa na ufanisi mdogo wa vyombo vya watumia maji na kuathiri uendelevu wa miradi ya maji vijijini.
Mhandisi Kasimbazi alisema , mkoa umechukua hatua za mikakati ya uboreshaji wa huduma za maji kwa kufanya utafiti wa vyanzo vya maji na kukamasisha uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa mabwawa madogo.
Alitaja mkakati mwingine ni kuendelea kutafuta vyanzo vingine vya fedha tofauti na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) ili kugharamia uendeshaji wa miradi ambayo imekwisha sanifiwa tayari .
Hata hivyo alisema kuwa, lengo ni kufikia wastani wa kitaifa la upatikanaji wa maji mijini kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020 na vijijini kwa asilimia 85.
No comments:
Post a Comment