Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za kutelekeza mtoto, baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha mtoto ambaye amefanana naye akitajwa kumtelekeza.
Msigwa amesema kwamba alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii anamaanisha hivyo na anamtaka mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa walioenda kwa mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kwa kutelekezwa, asiishie hapo tu bali aende hata Bungeni.
“Ilikoanzia imeanzia kwa Jerry Muro ndiye kasambaza hizi habari, kitu ambacho nakijibu hapa amekianzisha Jerry Muro, sasa mimi nasema kama huyo mtu yupo, nimetoa namba zangu na kama sipatikani aje hapa Bungeni”, amesema Peter Msigwa.
No comments:
Post a Comment