Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson akikata utepe kuashiria uzinduzi wa albamu mpya ya Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili. Rose Muhando ijulikanayo kwa jina la 'Usife Moyo'wakati wa kilele cha tamasha la pasaka katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana jioni.Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na mwandaaji wa tamasha hilo Alex Msama.
Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson kwa pamoja na viongozi wengine wakifurahia jambo mara baada ya uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando ijulikanayo kwa jina la 'Usife Moyo',.
Mgeni rasmi katika tamasha la pasaka 2018,Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson akizungumza mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),waliofika kushuhudia waimbaji wa nyimbo za injili wakitumbuiza katika tamasha hilo mapema jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.Dkt Tulia aliwaasa Watanzania kuilinda na kuitunza amani ya nchi kwa gharama yoyote,kwani wakiichezea amani waliyonayo kuipata tena haitakuwa rahisi,hivyo akaongeza kwa kuwaomba Watanzania waishi kwa upendo,kushirikiana kwa namna moja ama nyinine na pia kushiriki katika suala zima la kujenga uchumi wa nchi yao na hatimae kupiga hatua katia suala zima la maendeleo.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini,Mh.Anthony Mavunde akitoa neno la shukurani kwa kampuni ya Msama Promotions Ltd kwa kuandaa tamasha la pasaka 2018 mjini humo na kuwakusanya Wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake,kuja kujionea waimbaji mahiri wa nyimbo za injili ndani ya uwanja wa Jamhuri.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,Alex Msama ambaye ndiye Muaandaji wa tamasha la pasaka 2018 akiwashukuru wakazi wa Dodoma na Vitongoji vyake waliojitokeza kwa wingi katika tamasha la pasaka ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson,Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwajelwa pamoja na Rose Muhando.
Naibu Spika wa Bunge Mh. Dk. Tulia Ackson akicheza na Mwimbaji Rose Muhando, Mwimbaji Bonny Mwaiteje na Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwajelwa na baadhi ya wabunge mara baada ya kuzindua albam yake inayoitwa “Usife Moyo” kwenye tamasha la pasaka lililofanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana jioni.Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na mwandaaji wa tamasha hilo Bw. Alex Msama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora Mh. Kapteni George Mkuchika akizungumza katika tamasha hilo huku Naibu Spika Dk.Tulia Ackson na baadhi ya viongozi wengine wakimsikiliza.
Sehemu ya Meza kuu,ikifurahi yaliyokuwa yakijiri uwanjani huku waimbaji wakiendelea kuimba kwa zamu ndani ya tamasha la Pasaka jana jioni mjini Dodoma.
Sehemu ya Meza kuu ilipoamua kushuka na kwenda jukwaani kuunga mkono na kutoa neno la shukurani kufuatia kufanyika tamasha la Pasaka jana jioni mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment