ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 12, 2018

Orodha ya wanajeshi waliopandishwa cheo na Magufuli hii hapa

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akitangaza majina ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais John Magufuli amewapandisha vyeo maofisa wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) akiwamo Meja Jenerali Peter Massao aliyepandishwa kuwa Luteni Jenarali.
Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo leo Aprili 12, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maaofisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na maluteni jenerali wawili.
Wengine waliopandishwa vyeo na Rais Magufuli ni Brigedia Jenerali Henry Kamunde aliyepandishwa na kuwa meja jenerali.
Pia amewapandisha vyeo maofisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha kanali na kuwa brigedia jenerali na ofisa mmoja kutoka luteni kanali na kuwa kanali.
Waliopandishwa vyeo hivyo ni D.D.M Mullugu, J.J Mwaseba, A.S Mwamy, R.K Kapinda, C.D Katenga, Z.S Kiwenge, M.A Mgambo, A.M Alphonce, A.P Mutta, A.V Chakila, M.G Mhagama, V.M Kisiri, C.E Msolla na S.M Mzee.
Wengine ni C.J Ndiege, I.M Mhona, R.C Ng’umbi, S.J Mnkande, A.C Sibuti, M.M Mumanga, I.S Ismail, M.N Mkeremy, G.S Mhidze, M.A Machanga, S.B Gwaya, P.K Simuli na M.E Gaguti.

No comments: