JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO
WA AFRIKA MASHARIKI
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600
|
|
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES
SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO
Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za mafunzo ya muda mrefu
kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Pan African (PAU).
Mafunzo hayo ambayo yapo
kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu yatatolewa katika kozi
mbalimbali zikiwemo Baiolojia, Hesabu, Uhandisi, Sayansi ya Afya, Usimamizi wa
Mazingira, Sayansi ya Michezo, Mifugo, Uongozi na Mtangamano, Lugha, Ukalimani
wa Mikutano na Ufasiri, Uhandisi wa Maji na Nishati.
Kwa waombaji wa
Shahada ya Uzamili wanatakiwa kuwa na miaka isiyozidi 30 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 35 kwa waombaji
wanawake. Aidha, kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu wasiwe na miaka zaidi ya 35
kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 40 kwa waombaji wanawake.
Maombi ya mafunzo
haya yanatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia anuani ya barua
pepe ya pau-au.net. Mwisho wa kutuma maombi ya fursa hizi ni tarehe 20 Aprili,
2018. Maelezo ya ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia pau.scholarships@africa-union.org
au www.pau-au.net. Mratibu wa Mafunzo haya ni Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
18Aprili,
2018
No comments:
Post a Comment