Mkutano wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Biashara,Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea kufanyika jijini Arusha. Mkutano huu unafanyika kwa kipindi cha siku saba (7) kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018. Pamoja na mambo mengine yatakayojili, Mkutano huu unatarajia kufanya yafuatayo:-
- Kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maagizo na maamuzi yaliyofanywa na mkutano uliopita wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji;
- Kupokea na kajadili taarifa ya majadiliano ya awali ya bajeti ya Baraza la Mawaziri wa Fedha la Jumuiya ya Afrika Mashariki;
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Forodha
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Kisekta ya Biashara;
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Mamlaka ya Ushindani;
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Viwango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; na
- Kupokea na kujadili taarifa kutoka Kamati ya Kisekta ya Viwanda.
Mkutano huu anafanyika katika ngazi tatu ambazo ni ngazi ya waalam, ngazi Makatibu Wakuu, na ngazi ya Mawaziri.
Mkutano huu umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano ukiendelea |
No comments:
Post a Comment