ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 21, 2018

Taasisi ya Mo Dewji yatoa msaada kwa watoto wenye saratani

Taasisi ya Mo Dewji imetoa msaada kwa watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya saratani katika kituo cha Tumaini la Maisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Msaada ambao umetolewa ni unga wa ngano, khanga na sabuni za kuogea, kufua na kunawia mikono.

Akikabidhi msaada huo, Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul alisema taasisi yao itaendelea kuwa na utaratibu wa kutoa msaada katika kituo hicho ili kuwafariji watoto ambao wanapatiwa matibabu.

Alisema hiyo sehemu ya kwanza kutoa msaada kwani wamekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii kutokana na uhitaji uliopo hivyo kwa kufanya hivyo wanaamini watakuwa wamegusa maisha ya Watanzania wengi.

Aidha, Paul amewataka watu wengine wenye uwezo kuweka utaratibu wa kusaidia watu wengine wenye uhitaji kama watoto waliopo katika kituo cha Tumaini la Maisha.
Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto ambao wanapatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha.


Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasimamizi wa kituo cha Tumaini la Maisha wakati walipokuwa wakikabidhi msaada katika kituo hicho.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (USDM) ambao wanalipiwa gharama za masomo na Taasisi ya Mo Dewji wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaopatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha.

No comments: