ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 21, 2018

WAZIRI DKT KALEMANI AZINDUA USAMBAZAJI WA GESI ASILIA MAJUMBANI

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza katika uzinduzi wa usambazaji wa gesi asilia majumbani kwa mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara hafla iliyofanyika katika stesheni ndogo ya kupokea gesi hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Matiku Makori (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba. Picha zote na Cathbert Kajunason - Kajunason/MMG.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba akielezea hisitoria ya mradi huo na jinsi utakavyoweza wafaidisha wananchi watakafungiwa gesi hiyo asilia.
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Matiku Makori akitoa shukrani zake za pekee kwa shirika la TPDC kuwanzisha mradi utakaowaletea wananchi matokeo chanya ikiwa ni pamoja na kupunguza uharibifu wa mazingira.

Wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akipata maelezo jinsi mtambo unavyopokea gesi asilia na kuisambaza majumbani.
Mtambo wa kupokea na kusambaza gesi asilia.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akikagua moja ya nyumba ambayo imeshafungiwa gesi ya asili tayari kwa matumizi.
Moja ya mita ya kusoma gesi inapoingia nyumbani.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Matiku Makori wakiwasha jiko lililofungwa gesi asilia tayari kwa matumizi ya nyumbani katika eneo la Mikocheni mtaa wa TPDC jijini Dar es Salaam.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amezindua usambazaji wa gesi asilia kwa mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara na hivyo kutoa fursa wanananchi wa mikoa hiyo kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 40 kutokana na gesi ya mitungi inayotumiwa majumbani Dkt. Medard Kalemani, amesema kuanza kwa matumizi ya gesi hiyo kutawasaidia wananchi wa mikoa hiyo na hususani wa jiji la Dar es Salaam, kupunguza gharama kwa asilimia 40, ikilinganishwa na gharama ya matumizi ya mitungi ya gesi inayotumiwa na wananchi wengi hivi sasa. Dkt Kalemani amesema usambazaji huo wa awamu ya kwanza unaofanywa kuanzia eneo la Ubungo mahali ambapo kwenye kituo cha gesi hiyo kutokea Mtwara, utaigharimu Serikali kiasi cha Sh Bilioni 4 zitakazotumika kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali kutoka eneo hilo hadi itakapopelekwa. Ameyataja maeneo ambayo usambazaji wa gesi hiyo kwa awamu ya kwanza utafanyika kuwa ni pamoja maeneo yote ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ubungo, Survey, Makongo juu, Sinza, Mikocheni, Mwenge, Tegeta hadi kiwanda cha Sao Hill. Pamoja na maeneo hayo, mengine ni pamoja na maeneo ambayo gesi kutoka Ubungo hadi Gereza la Keko itapita, Ubungo hadi Mbagala, pamoja na maeneo ya Kimara hadi Tabata, huku Waziri huyo akimuagiza Mkandarasi aliyepewa kazi ya usambazji wa gesi hiyo kukamilisha kazi hiyo ifikapo Septemba Mwaka huu. Aidha amesema awamu ya pili ya usambazaji huo inatarajiwa kuanza Julai mwaka huu huku akitajwa kuigharimu Serikali kiasi cha Sh Bilioni 11, ambapo usambazaji huo utafanywa katika maeneo ya Kigamboni pamoja na Mkuranga na kwingineko ndani ya Jiji la Dar es Salaam. “Hatua hii inakwenda kumaliza suala la matumizi ya nishati ya mkaa ambapo inakadiriwa kuwa asilimia tisini (90%) ya wananchi wa Dar es Salaam wanaitumia na hivyo kuchangia uharibufu wa mazingira pamoja na misitu, imani yetu matumizi ya gesi asilia yatasaidia kuleta mageuzi makubwa ya nishati hapa nchini” amesema Dkt Kalemani. Pamoja na hayo amesema umeme unaozalishwa kupitia mitambo ya Kinyerezi 2, Kinyerezi 3 uliopo katika matengenezo pamoja na mtambo wa Somangafungu unaotarajiwa kuzalisha Megawati 330 kuanzia mwaka ujao, kwa pamoja itasaidia kuzalisha zaidi ya Megawati 2,780 za umeme. Amewataka wenye viwanda kukaa tayari kwa ajili ya kuunganishiwa nishati hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam huku akimtaka mwekezaji wa kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kuomba kuunganishiwa nishati hiyo ‘hata leo’ Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba, amesema maandalizi kwa ajili ya usambazaji wa gesi hiyo katika maeneo yote yaliyoainsihwa katika mpango wa awali umekamilika na kwamba kinachofuata sasa ni kuwaunganishia wananchi nishati hiyo. Alisema ukiacha uunganishaji wa gesi hiyo kwa wananchi, pia wataviunganishia viwanda viliwili vilivyopo eneo la Mikicheni, kikiwemo kiwanda cha Wazo pamoja na IPTL.

1 comment:

Anonymous said...

Ni hatua nzuri lakini rai yangu ni kuwa hii ni serious and very dangerous undertaking tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa katika kumaintain hiyo distribution infrastructure otherwise itakuwa ni balaa.