Klopp mwenye miaka 50, amekuwa chaguo la kwanza kwa Rais huyo wa klabu tajiri nchini Hispania, huku Perez akisisitiza kuwa ndiye mwenye sifa na mwonekano wa kutua kwenye kikosi hicho cha Bernabeu.
Mfanikio ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya yamechangia kumuweka sokoni kocha huyo baada ya kucheza fainali ambayo hata hivyo waliishia kulimwa mabaop 3-1.
Klopp alitua kwenye kikosi cha Liverpool mwaka 2015 akirithi mikoba ya Brendan Rodgers kwenye dimba la Anfield.
Hata hivyo, baada ya ofa hiyo kutolewa, Liverpool wanapambana kumbakisha kocha huyo ambaye bado ana mkataba uliosalia wa miaka minne.
Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment