Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wasafi TV kuunganishwa kwenye king’amuzi cha Startimes katika ukumbi wa Hotel ya Slipway jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la WCB wamezungumza kuhusu baadhi ya vyombo vya habari kutopiga nyimbo za wasanii wao.
Miongoni mwa mameneja wa WCB, Babu Tale katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana alisema kwa vile vyombo hivyo viliwakataa mwanzo na sasa waendelee hivyo hivyo.
‘Tunaendelea kuwaomba waendelee kushinikiza wafanyakazi wao wasipige nyimbo zetu..
“Hatutaki kuona wanapiga nyimbo zetu wala kutoa habari zetu kwa sababu wao walitukataa mwanzo, tunawakataa kwa sababu wao walitukataa,” alisema Babu Tale kwa msisitizo.
Hapo awali Diamond Platnumz alisema siku zote katika tasnia mbalimbali michezo ya kubaniana ipo ila hawezi kulaumu.
Diamond alisema kufuatia hatua hiyo iliyochukuliwa na vyombo hivyo iliwapa nguvu timu nzima ya Wasafi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuwasaidia wasanii wengine ambao wanakutana na changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment