ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 19, 2018

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ALIPOTEMBELEA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT), TAASISI YA SEKTA BINAFSI TANZANIA (TPSF) NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN HAPA NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kushoto akipokea zawadi ya mtungi wa kiasili kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika ofisi ndogo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam leo. Picha na Mpiga Picha Wetu. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza na watendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kuhusu mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya sekta za mifugo na uvuvi alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa TPSF, Godfey Sembeye. Picha na Mpiga Picha WetuWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) na Naibu Gavana wa Benki Kuu anayeshughulikia Uchumi na Fedha, Dk. Yamungu Kayandabila mara baada ya kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa benki hiyo alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akifurahia jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya BOT Dar es Salaam .
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akiagana na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dar es Salaam

No comments: