Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, (katikati), akikokota mpira wakati wa pambano
la soka kwenye mazoezi yaliyowashirikisha washiriki wa mafunzo kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa migogoro
itokanayo na kazi (CMA) kwenye
uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo Agosti 16, 2018.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, amehimiza ushirikiano wa kitaasisi
katika Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuongeza ufanisi wa kazi.
Mhe. Mvunde alitoa rai hiyo leo
asubuhi Agosti 16, 2018 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuongoza
mazoezi yaliyoambatana na michezo mbalimbali ya washiriki wa mafunzo ya kujenga
uwezo kwa watumishi wa Tume ya Usuluhishi
na Uamuzi wa migogoro itokanayo na kazi (CMA).
“Napongeza ushirikiano huu
mliouonyesha kuwezesha mafunzo haya, nawapongeza WCF, na taasisi nyingine
mlizoshirikiana nazo katika kutoa mafunzo haya muhimu kwa wafanyakazi wetu,
ushirikiano huu ni muhimu kwani wote mnatumikia Ofisi ya Waziri Mkuu.” Alisema
Mhe. Mavunde.
Aliipongeza Tume kwa kufanya
mabadiliko makubwa katika kupunguza kero baada ya kuja na mkakati wa kupunguza
muda katika kufanya usuluhishi. “Hivi sasa mnaanza kuturejeshea heshima ya tume
yetu, mimi huwa nashiriki vikao vya wadau wa viwanda na biashara na moja ya
changamoto kubwa waliyokuwa wanaisema ni kwenye masuala ya usuluhishi na uamuzi
(CMA), kesi zinachukua muda mrefu sana, haziishi kwa wakati na hivyo
kuchelewesha ukuaji wa uchumi wa viwanda, lakini haya yalisemwa miaka miwili
ile ya mwanzo lakini hivi sasa naona kuna mabadiliko.” Alisema.
Alisema hadi hivi sasa mashauri 9,379
ambayo yalikuja kwa ajili ya usuluhishi, mashauri 7,017 sawa na asilimia 78%
yameshughulikiwa na kuamuliwa.
“Haya ni maendeleo makubwa na hii ndiyo
iwe spirit ya tume kuona namna bora
ya kuweza kuharakisha usuluhishi na uamuzi ili Watanzania wapate haki zao
lakini vile vile isaidia kuharakisha huu uchumi wa viwanda ambao kila mmoja
tunaamini kwamba ifikapo mwaka 2025 imani ya serikali ni kwamba uchumi wa
viwanda utaajiri zaidi ya asilimia 40 ya nguvukazi ya watu milioni 22.3 waliopo
Tanzania.” Alisema.
Awali Mhe. Naibu Waziri aliongoza
mazoezi ya viungo, mchezo wa soka, kufukuza kuku, kuvuta kamba, kukimbia na
magunia.
Mafunzo hayo yameratibiwa na CMA kwa
ushirikiano na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mshindi wa kukimbiza kuku kundi la Wanawake, akiondoka na kuku wake.
Mbio za kuku.
Mchezo wa kuvuta Kamba.
Mchezo wa kuvuta Kamba wanawake
No comments:
Post a Comment